• Harusi yao ilitia ushawishi kwa sababu ilifanyika katika barabara ambapo wapita njia na wafanyi biashara wangeweza kushuhudia harusi hiyo.
• Wawili hao waliweza kubadilishana viapo mbele ya mashabiki wao,katika sehemu amabapo walikutana mara ya kwanza (Archives).
Tony Sherman na Kendi,wapenzi ambao walipata umaarufu baada ya kukutana katika maandamano ya kupinga serikali na kupendana, sasa wameolewa rasmi.
Kendi na Sherman walipatana wakati wa maandamano ya kupinga serikali na baada ya miezi mitatu Sherman alipendekeza ambapo Kendi alikubali.
Wanandoa hao walioana katika sherehe ya umma siku ya Jumapili, Agosti 25 katika jiji la Nairobi.
Harusi yao ilitia ushawishi kwa sababu ilifanyika katika barabara ambapo wapita njia na wafanyi biashara wangeweza kushuhudia harusi hiyo.
Wawili hao waliweza kubadilishana viapo mbele ya mashabiki wao,katika sehemu amabapo walikutana mara ya kwanza (Archives).
Pia walipanda farasi na kufanya kumbukumbu nzuri pamoja na mashabiki wao ambao walijitokeza kwa ajili yao.
Kwenye mtandao wa kijamii ( Instagram) Sherman ameandika "Nimeoa rasmi....Ilikuwa na mafanikio...@terencecreative mkuu sasa fanya ile kitu....The Sherman's....Mungu aweke ndoa hii mahali bora."
Harusi hii imefanyika siku tatu baada ya Terence Creative kuahidi kusaidia safari ya mwanzo ya harusi ya Tony Sherman na Kendi.
Terence alisema atasaidia kushirikiana na Bonfire Adventures ili kutuma wanandoa hao Mombasa baada ya harusi.