•Bintiye Mike Sonko,Sandra Mbuvi,almaarufu Thicky Sandra ,amezua gumzo mitandaoni ,baada ya kusema kuwa yeye huoga mara tatu kwa siku.Sandra ,upande mwingine ,amesema kuwa yeye hawezi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume Mkenya kwa alichodai kuwa hawana pesa za kutosha
Sandra Mbuvu mwanawe aliyekuwa gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko ameeleza kuwa yeye huoga mara tatu kwa siku.
Ni jambo ambalo limezua gumzo mitandaoni,huku Wakenya wakitoa kauli za kejeli.
Sandra alionekana kusisitiza kuwa usafi ni muhimu muhimu licha ya kusema kuwa Wakenya watona ni mzaha kwamba yeye huoga mara tatu kwa suku,"Naoga mara tatu kwa siku'
Sandra Mbuvi almaarufu Thicky Sandra,alipokuwa akihojiwa na Obinna TV,alieleza kwamba yeye hayuko tayari kuwa kwenye mahusiano na mwanaume wa Kenya kwa alichosema kuwa wanaume Wakenya ni fukara.
"Napenda wanaume warefulakini waaminifu,Mimi siwezikudate Mkenya,sitaki wanaume fukara".
Aidha ,Sandra alielezea kuwa mahari yake ya mahari ni:"Bei yangu ya mahari ni Bentley 22,simba 7,pauni milioni 500 pesa tasilimu ,chopa na ndege,lions ni za kunichunga".
Haya yanatokea siku chache baada yake kusema kuwa nambari yake ya simu uuza kwa pesa za Kenya 2500 ili mtu kuwa nayo.Ni jambo ambalo lilizua gumzo mitandaoni ,uku wakenya wakionekana kutamaushwa na jambo hilo.Na wengi wa Wakenya katika mitandao ya kijamii hasa wanaume,wakitoa kauli zenye uzito,"alafu nani atatoa hiyo mahari yote kwa mkamba"
Aidha,wengi wa Wakenya mitandaoni ,walisema kuwa Sandra amejipandisha cheo sana ,na ni heri watumie hela zao kwa jambo lingine lakini sio,kununua nambari yake.