Video Mama akimfokea mwanawe kwa kumtongoza mrembo kanisani yazua minong’ono

Mazungumzo yao yanaposonga mbele, kijana huyo anampa bibi huyo simu yake ili aiweke nambari yake ya simu ili waendelee na urafiki nje ya kanisa.

Muhtasari

• Mazungumzo yao yanaposonga mbele, kijana huyo anampa bibi huyo simu yake ili aiweke nambari yake ya simu ili waendelee na urafiki nje ya kanisa.

kuomba namba kanisani.
kuomba namba kanisani.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameanza kutoa maoni yao kufuatia video mpya ambapo mama anamdhalilisha hadharani mwanawe wac kiume aliyekomaa kisa alijaribu kuomba namba ya simu ya mrembo wakati wa ibada.

Klipu hiyo inayovuma iliangazia wakati mvulana huyo alipokuwa ameketi kando ya mwanamke wakati wa ibada ya kanisa na kwa muda mrefu akaanza kuwa na mazungumzo ya chinichini naye.

Mazungumzo yao yanaposonga mbele, kijana huyo anampa bibi huyo simu yake ili aiweke nambari yake ya simu ili waendelee na urafiki nje ya kanisa.

Akiwa anajua mwanae anachofanya na bibi huyo, mama huyo anatoka kwenye kiti chake cha nyuma cha mbali na kuelekea kwenye kiti cha mwanawe na kumnyang'anya simu mwanadada huyo.

Aliendelea kumuendea mwanae kwa nguvu huku akimfokea kanisani, jambo ambalo baadaye lilimfanya kijana huyo kulia huku akionekana kuvua glasi yake kujifuta machozi.

Wakati huo mwanadada huyo alibaki katika hali ya mshangao na hakuweza kusema neno lolote huku akiwa haamini tena macho yake kufuatia kile ambacho mama huyo alichomfanyia mwanae aliyekua akijaribu kumvutia.

Tazama video hapa chini;