•Pastor Kanyari ashauriwa na mwanawe msichana (Sky) kuwa anafaa kuoa mara ya pili jinsi mama yake alivyofanya.
•Sky aliweza kufanya baba zake wawili kukutana
•Hiram Gitau ni baba wa kambo wa Sky Victor na Danny
•Hiram alipeleka wanawe wawili kuona baba yao mzazi Kanyari.
Huenda Kanyari akaoa mara ya pili baada ya mwanawe, Sky kumsauri kuoa tena.
Katika video iliyoshirikishwa Youtube na mwanawe Sky Victor, Sky alikuwa anataka baba zake wawili (Kanyari na Hiram) wakutane kwani hawajawai patana tangu mama yao kuoa baba wa kambo.
Badala ya msaidizi wao wa nyumba kuwapeleka kwa baba yao mzazi kama kawaida, Sky aliweza kumshauri baba yao wa kambo kuwapeleka.
Kanyari alisikika akikiri kuwa hajawai patana na Hiram.
"Umeniletea hawa...for the first time tumemeet..hatujawai meet mi nakuonanga tu...for the first time tunaonana uso kwa uso...I have never seen him with my eyes lakini nakuskianga”
Sky alikuwa anataka baba zake wawili wakutane hata kama alikuwa na hofu ya wao kupigana.
Kanyari pamoja na msaidizi wake wa kibinafsi Baby Benson alikuwa akipeleka wanawe Sky Victor na Danny Village Market kuburudika.
“Baba nadhani unafaa kuoa tena kwa sababu unajua mama aliolewa tena kwa hivyo unafaa kuoa tena...you don't be odd one out..nadhani unafaa kuoa Baby. Unajua huwa wanasema mama wa kambo ni wabaya na Baby ni mzuri" Sky alimwambia babake.
Sky tena alimuuliza babake kama akioa atawacha kuwapenda ambapo Kanyari alisema hapana.
Victor Mwangi Kanyari ambaye anajulikana kama Pastor Kanyari ni mhubiri kiongozi wa Salvation Healing Centre.
Alikuwa mume wa zamani wa Betty Bayo ambaye walipata watoto wawili (Sky Victor na Danny).
Beatrice Mbugua alamaarufu Betty Bayo ni msanii wa ngoma za injili ambaye ameolewa tena na Hiram Gitau.