"Ndoa ni UTAPELI!" Vera Sidika aapa kutowahi kuolewa tena baada ya ndoa ya kwanza kufeli

Sosholaiti huyo alisema kwamba baada ya kuonja jinsi ndoa ilivyo, hataki kuifanya tena.

Muhtasari

•Vera alichapisha video ya kumbukumbu yake akiongea kuhusu kutotaka kuolewa wakati wa mahojiano ya zamani ya TV.

•Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

Vera Sidika
Vera Sidika
Image: HISANI

Mwanasosholaiti maarufu wa Kenya Vera Sidika ameweka wazi kuwa hataki kuolewa tena.

Siku ya Jumapili, mama huyo wa watoto wawili alichapisha video ya kumbukumbu yake akiongea kuhusu kutotaka kuolewa wakati wa mahojiano ya zamani ya TV.

Katika posti yake, aliendelea kusisitiza kuhusu hisia zake za zamani, akisema kwamba baada ya kuonja jinsi ndoa ilivyo, hataki kuifanya tena.

"Hii ilikuwa miaka 8 iliyopita. Siku zote nilisema sitaki kuolewa, sijui ni nini kilitokea wakati wa Covid lakini nimekuwa huko na niamini: Ndoa ni UTAPELI!!! Sitaki tena!.” Vera aliandika chini ya video aliyoiweka kwenye Instagram.

Haya yanajiri zaidi ya mwaka mmoja baada ya sosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 34 kuachana na mzazi mwenzake Frederick Mutinda almaarufu Brown Mauzo.

Mwishoni mwa Agosti mwaka jana, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"