Wapenzi wa Maadamano waomba wakenya msaada kwenda Mombasa

Tony Sherman na Kendi wanaomba @bonfireadventures kuwapeleka Mombasa

Muhtasari

•Wanandoa wa maandamano wanaomba mkenya yeyote kufadhilia honeymoon yao ili waende Mombasa kwani imekuwa wiki moja na zaidi tangu wafanye harusi katika jiji la Nairobi lakini hawajafaulu kusherekea honeymoon yao

Tony Sherman, Kendi
Tony Sherman, Kendi
Image: Tony Sherman//Facebook

Tony Sherman na Kendi wanawaomba Wakenya msaada ili waweze kwenda Mombasa kwa safari ya mwanzo wa harusi.

Kendi na Sherman walifanya harusi Jumapili Agosti 25 katika jiji kuu la Nairobi wakiwa na matumaini ya kwenda Mombasa kusherekea safari yao ya mwanzo wa harusi baada ya harusi.

Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii,Tony Sherman na Kendi waliandika kuwa wiki moja na zaidi imepita tangu wafanye harusi katika jiji la Nairobi na kuomba mkenya yeyote kujitolea ili kufadhilia honeymoon yao.

Pia walisema kuwa wanampango wa kuwasaidia watoto wa mitaani hata kama ni kwa upendo mwingi.

"My wife and I are pleading with any willing Kenyan to sponsor our honeymoon, it's been one week plus since we did our wedding in the Nairobi CBD...@bonfireadventures please take us to Mombasa...We also have plans of giving back to the streets since that's where we found love it has also been our biggest dream...to help street children even with lots of love."

Wanandoa hawa walifanya harusi katika jiji la Nairobi ambalo lilihudhuriwa na mashabiki wao na kushuhudiwa na wafanyi biashara kwa sababu ilikuwa harusi ya umma.