Ndrendende aeleza maisha ya Kamiti

Mfungwa wa zamani Ndrendende alifungwa kwa miaka 10 na miezi 6 baada ya kushikwa alipokuwa ametoka kazi

Muhtasari

•Ndrendende aeleza alivyoshikwa  na kufungwa kwa miaka 10 na miezi 6 na kuachwa huru mwaka wa 2014

•Ameweza kusema njia mbalimbali ambazo watu hutumia kuishi jela

Ndrendende na rafiki
Ndrendende na rafiki
Image: Eric Ndre//Facebook

Mfungwa wa zamani Eric Oduor a.k.a Ndrendende, amesimulia jinsi alivyoshikwa na kufungwa jela kwa miaka 10 na miezi 6 na alivyofaulu kuwachiliwa huru.

Ndrendende anasema kuwa alishikwa alipokuwa ametoka kazi akielekea nyumbani kwake. Alishikwa kwa madai ya kuibia Chifu.

Alipelekwa katika kituo cha polisi na kukalisha siku kumi uchunguzi ukifanywa. Baada ya siku 14, alifikishwa kortini ambapo alikana madai ya wizi ambayo alikuwa amedaiwa kufanya na baadaye kufikishwa Kamiti.

Kwa jela chawa ni kitu cha kawaida na ukionekana ukiziua ni hatia.

"Chawa ni afande jela hakuna kuua chawa...huyo ndio anakuchunga usiku usilale."

Kuna njia mbalimbali za kuishi jela "Jela ndio mahali mtu anaweza pretend kwa miaka 20 ati ni kiwete na sio kiwete ndio akule mchele kwa maharagwe," Ndrendende alisema.

Vyoo ni viwili na havina milango kwa madai ya kuwa wafungwa wanaweza toroka.

"Choo ni open air...huwezi jifungia...ndio usitoroke... na ni choo mbili...hiyo line ndiyo bado ya uji...unaenda choo na sahani yako kwa mkono"

Alipoulizwa namna ya kujipangusa baada ya kujisaidia alisema kuwa watu wanatumia maji na ni yeye pekee alikuwa anajipangusa sababu alikuwa spika alikuwa analeta wageni na malipo yake ilikuwa lazima umpe sabuni moja ama karatasi shashi moja.

Jela mwenye alikuwa anajipanguza pekee yake ni mimi”

Wafungwa wanapenda soap opera kwa sababu wamehukumiwa kwa miaka mingi, wanataka kitu ambacho wanaweza fuatilia.

Jela nunua vitu viwili: ndoo mbili na matress ndogo pekee. Ndoo moja ni choo ambayo hutumiwa usiku wakati wa lock up na ingine ni ya maji ya kunywa.

Anasema kuwa jela ni mahali ambapo mtu hawezi toroka sababu zikiwa nyingi moja wapo ni kuwa kuta ni ndefu na nyingine ni kuwa imezungukwa na kambi ya Kenya Prison.

Anasema ni muhimu sana kuwatembelea wale walio jela kwani ukiwaachilia huko sana wanakosa matumaini na kuona maisha yao yameisha hivi  kujipata wanategemea wenzao.

 Ndrendende  alikuwa amehukumiwa kifo lakini aliwachwa huru mwaka wa 2014 baada ya upande wa mashtaka kukosa ushahidi.

Sahii yeye ni mtu wa kujitolea ambaye anawashauri vijana waachane na mambo ya uwizi na madawa za kulevya.