Mhubiri Dan Wema akataa ombi la ndoa kutoka kwa mwanadada

Wema alipata ujumbe huo na kujibu aaachwe afanye kazi ya Mungu kwanza.

Muhtasari

•“Naitwa Agnes ninampenda mtume Dan Wema. Tafadhali, je utanioa?. Nina umri wa miaka 27,” bango hilo lilisoma.

•“Hadi shangazi yangu mmoja amenitumia hii picha aiiii. Watu wa Nairobi achaneni na mimi,” Wema aliandika.

Mtume Dan Wema
Mtume Dan Wema
Image: DAN WEMA//Facebook

Mhubiri Dan Wema amekataa ombi la ndoa kutoka kwa Agnes baada ya mwanadada huyo kukiri kuwa anampenda na angependa kuolewa na yeye.

Picha imekuwa ikisambaa mtandaoni ya mrembo mmoja akiwa amebeba bango ambalo aliandika akikiri anampenda mtumishi huyo wa Mungu.

Kwenye bango, mrembo huyo alijitambulisha kama Agnes mwenye umri wa miaka 27 na kukiri kuwa anampenda Wema na kumuuliza kama atamuoa.

“Naitwa Agnes ninampenda mtume Dan Wema. Tafadhali, je utanioa?. Nina umri wa miaka 27,” bango hilo lilisoma.

Wema alipata ujumbe huo na kujibu aaachwe afanye kazi ya Mungu kwanza na kuomba kuacha kutumiwa picha hiyo.

Acha nifanye kazi ya Mungu tu kwanza... Usinitah kwa hii picha tafadhali...Ni sawa ni vizuri mtu kujieleza na amejieleza. Lakini usinitumie picha hii,"

Alisema kuwa mmoja wa shangazi yake amemtumia picha hiyo na akawataka watu wa Nairobi kuachana naye.

Hadi shangazi yangu mmoja amenitumia hii picha aiiii. Watu wa Nairobi achaneni na mimi,” Wema aliandika.

Hii sio mara ya kwanza mwanadada kubeba bango na kukiri kuwa anampenda mwanamume flani.

Wiki moja iliyopita madada wawili kutoka Nakuru walikiri kuwa wanampenda Bradley na wako tayari kuishi na yeye maisha yao yote.

Raquel Kirika na Mary Kirika kama walivyojitambulisha, walitumia bango kufikisha ujumbe wao kwa kijana huyo mrefu wakisema wanajitoa kwake.

Kulingana na wao, Bradley anastahili wanawake wawili warembo na wameweka wazi kuwa wako tayari kuishi maisha yao yote naye.

"Sisi ni dada kutoka Nakuru, Raquel na Mary Kirika. Tuliketi na kuamua kijana mrefu na mwenye sura nzuri anastahili wanawake wawili warembo kando yako kukaa nawe maisha yako yote," wawili hao walisema kwenye bango hilo ambalo walishikilia.

Image: Screenshot