Muundaji wa maudhui ya kidijitali na mwanamitindo Joanna Kinuthia amefichua kwamba penzi lake na Chris Kaiga limechipuka upya, miezi mitatu baada ya kuthibitisha kuachana kwao.
Mnamo Julai, mrembo huyo kupitia kwa kipindi cha maswali na majibu kwenye Instagram, alithibitisha kwamba yeye na msanii Chris Kaiga walikuwa wameachana.
Hata hivyo, siku moja iliyopita, alimjibu shabiki mmoja ambaye alitaka kuthibitisha macho yake kile alichokiona, na Kinuthia akamjibu akisema kuwa ni kweli macho yake hayakuwa yamemdanganya.
Shabiki huyo alimuuliza kama ni kweli aliyemuona naye ni Chris Kaiga na Joanna Kinuthia akathibitisha kwamba ni kweli, kwani walisharudiana kinyemela.
“Ni kama nimeona Chris Kaiga?” Shabiki huyo kwa jina Kanjiruu alimuuliza kwa utani.
“Tulirudiana” Joanna Kinuthia alimjibu. Joanna na Chris walithibitisha kuwa walikuwa ‘mwili mmoja’ wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwa mrembo huyo mwenye umri wa miaka 27 mnamo 2022. Lilikuwa tukio la karibu sana nyumbani kwake na familia yake na marafiki wa karibu.
Alishiriki video ya wawili hao katika busu la mapenzi ambalo liliwaacha mashabiki wakiwa na mbwembwe kwani walificha mambo kwa muda mrefu.
Hata hivyo, katika hali ya kutamausha, miaka miwili baadae, Joanna Kinuthia alitoa taarifa mbaya kuhusu kuachana kwao, akisema kwamba alikuwa ameachana na msanii huyo kwa takribani mwezi bila mtu yeyote wa nje kujua.
Katika Maswali na Majibu kwenye hadithi yake ya Instagram iliyopewa jina la `Niulize kitu' ili kujaribu kuungana na wafuasi wake, alijibu moja ya maswali ya mashabiki wake walioandika, "I Love your honesty."
"Nimepata maswali machache kuhusu hili, hauchapishi Chris tena, nyie bado mko pamoja? Ukweli ni hapana, hatuko pamoja tena, "alisema mtayarishaji wa maudhui.
"Imekuwa muda, kama zaidi ya mwezi sasa. Niko sawa guys imagine niko sawa. Sijui niseme nini zaidi kuhusu hali hiyo.”
Hata hivyo, katika muda wote wa muendelezo kuhusu kumwagika kwa penzi lao, msanii Chris Kaiga hajawaqhi lizungumzia suala hilo kupitia kwa mahojiano au kwenye kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii.