logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Toa hii bonoko sasa, nikuvalishe hii mzuri, Baba Jimmy amzawidi Mama Jimmy

Baba Jimmy azidisha mapenzi kwa mkewe Mama Jimmy

image
na Brandon Asiema

Dakia-udaku27 October 2024 - 15:02

Muhtasari


  • Wawili hao maarufu kama Mama Jimmy na Baba Jimmy walihamia Marekani mapema mwaka huu pamoja na watoto wao wawili.
  • Baba Jimmy alimweleza mkewe jinsi anampenda akimwomba waishi pamoja kwa miaka mingi katika upendo wa Mungu.

caption


Wanandoa waliotikisa mitandao ya kijamii nchini Kenya haswa tik tok kutokana na mapenzi yao ya kipekee, wameendeleza mapenzi ya hali ya juu hata baada ya kuhamia Marekani.

Wanandoa hao ambao mwanamume ni Mzungu na mkewe ni Mluhya kutoka Bungoma, wamesherekea kuishi pamoja kama mume na mke kwa miaka saba sasa na waemjaliwa na watoto wawili.

Katika maadhimisho yao ya miaka saba ndoani, Baba Jimmy amebadilisha pete aliyompa mke wake mara ya kwanza akisema kuwa amenunua zawadi nyingine mpya yenye bei ghali kitu amabcho alisema kuwa tangu waoane wamekuwa na pete rejareja ya shilingi ishirini.

Tangu tuoane tumetafuta pete zile za reja reja za shilingi ishirini, ama shilingi mia moja ama ata mia tatu lakini nimeamua kwa maadhimisho yetu ya miaka saba nikutafutie pete tu ya ukweli.” Alisema Baba Jimmy.

Mama Jimmy hakuficha furaha yake machozi ya furaha yalipomndokoka huku akimwombea mumewe baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Baba Jimmy alimweleza mkewe jinsi anampenda akimwomba waishi pamoja kwa miaka mingi katika upendo wa Mungu.

“Mimi nakupenda. Mama, tukae pamoja kwa upendo miaka mingi ya maisha yetu. Ninakupenda sana na Mungu anakupenda sana na upendo wake hata ni zaidi kuliko yangu lakini mimi nae nakupenda zaidi.” Alisema Baba Jimmy.

Wawili hao maarufu kama Mama Jimmy na Baba Jimmy walihamia Marekani mapema mwaka huu pamoja na watoto wao wawili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved