Amira amkejeli ex wake Jimal Rohosafi baada ya kuonyesha upendo kwa Kinuthia

Jimal alimueleza Kinuthia jinsi anavyoipenda kazi yake na kumtaka aendelee kuweka bidii zaidi.

Muhtasari

•Baba huyo wa wavulana wawili alimueleza Kinuthia jinsi anavyoipenda kazi yake na kumtaka aendelee kuweka bidii zaidi.

•Amira alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuchapisha meme iliyoambatana na ujumbe ambao ulionekana kuwa shambulio lisilo la moja kwa moja kwa Jimal.

Amira na aliyekuwa mumewe, Jamal Rohosafi
Image: INSTAGRAM

Mfanyibiashara Being Amira amefanya kile kinachoonekana kuwa shambulio lisilo la moja kwa moja kwa mume wake wa zamani Jimal 'Marlow' Rohosafi baada ya kuonyesha upendo kwa tiktoker maarufu Kelvin Kinuthia.

Jimal ambaye ni mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki wa Matatu jijini Nairobi mapema wiki hii alituma maneno ya kutia moyo kwa Kinuthia kupitia Instagram, tiktoker huyo ilionyesha screenshot ya mazungumzo yao.

Baba huyo wa wavulana wawili alimueleza Kinuthia jinsi anavyoipenda kazi yake na kumtaka aendelee kuweka bidii zaidi.

"Endelea kusukuma, unafanya vyema usiache. Napenda unachokifanya, ukiwa na shauku siku moja itajipa," Jimal aliandika.

Kinuthia alisherehekea ujumbe huo kwa bashasha tele na kueleza jinsi ulivyomtia nguvu ya kuendelea kupambana. 

"Kuamka na kuona maandishi kama haya kutoka kwa mtu ambaye amefanikiwa maishani hunipa nguvu sana.

Waah, asante sana Jimal Rohosafi imenitia moyo sana kaka," aliandika chini ya screenshot ya mazungumzo yake na mfanyibiashara huyo.

Baadaye siku ya Alhamisi, Amira alizamia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuchapisha meme iliyoambatana na ujumbe ambao ulionekana kuwa shambulio lisilo la moja kwa moja kwa baba huyo wa wanawe wawili.

Chini ya meme hiyo inayoonyesha mwanamume aliyesikitishwa, mfanyibiashara huyo aliandika "Awuoro 🏳️‍🌈,"

Bendera ya rangi za upinde wa mvua  (🏳️‍🌈) mara nyingi huhusishwa na jamii ya wapenzi wa jinsia moja (LGBTQ).

Ndoa ya Jimal na Amira ya muda mrefu ilisambaratika mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya Jimal kuonekana kumchagua aliyekuwa mkewe wa pili, mwanasoshalaiti Amber Ray, badala ya mkewe wa kwanza.

Julai mwaka jana, Jimal alikiri kujuta kusababisha kuvunjika kwa ndoa yake na kuomba msamaha kutoka kwa Amira.

Mfanyibiashara huyo  alikiri kuwa alimkosea sana mama huyo wa wanawe kwa kuingiza drama nyingi kwenye ndoa yao.

"Naomba radhi kwa kukukosea heshima, kukuaibisha, kwa kukuumiza, kwa maumivu yote na kwa huzuni niliyokuletea. 💔Samahani kwa nyakati zote ambazo sijawa mwanaume niliyeahidi kuwa," alisema.

Pia alikiri kuwa alikosa kutimiza  wajibu wake wa kumlinda mkewe kama alivyohitajika kufanya. Alisema kwamba alifahamu wakati ndoa yake ikiporomoka ila akashindwa na la kufanya kwa wakati ule.

"Ilikuwa mbaya kabisa. Huenda nilionekana kama mtu asiye na wasiwasi lakini sikuwa na la kufanya. Nilijua haikuwa sawa, nilijua unaumia lakini sikuweza kujikusanya!Amira nafanya hivi kwa sababu ukosefu wa heshima pia ulikuwa mkubwa. Naomba radhi kwa kukosa heshima," Aliandika.

Jimal pia alikiri kwamba hajakuwa sawa tangu alipokosana na mke huyo wake na mama ya watoto wake.

Katika jibu lake kwa ombi hilo la msamaha Amira hata hivyo alidokeza kuwa anahitaji muda kwani "vidonda vingine haviponi."