Betty Kyallo amtambua jamaa aliyeonyesha mahaba yake makubwa kwake

"Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya Betty Kyallo yalikuwa na wakili Nick Ndeda," Bango hilo lilisoma.

Muhtasari

•Betty alichapisha picha ya jamaa mmoja akiwa ameshikilia bango lenye maandishi matamu ya kumsifu.

•Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya Betty Kyallo yalikuwa na wakili Nick Ndeda.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Mwanahabari na mjasiriamali mashuhuri Betty Kyallo amemtambua mmoja wa wanaume Wakenya wanaommezea mate.

Kwenye Instastori zake, Betty alichapisha picha ya jamaa mmoja akiwa ameshikilia bango lenye maandishi matamu ya kumsifu.

"Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya Betty Kyallo yalikuwa na wakili Nick Ndeda. (Mrembo, Fasaha, Mpole, Mzuri, Mtamu)," bango hilo lilisoma.

Pichani, jamaa huyo alikuwa amevalia suruali nyeusi na T-shati nyeusi iliyoandikwa 'Mr Rhymer'.

Chini ya picha hiyo, Betty kwa utani alisema  "Wakenya wenzangu, habari ya asubuhi😅."

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mama huyo wa binti mmoja kudokeza kuhusu kuwa kwenye mahusiano mapya.

Hivi majuzi, mtangazaji huyo alichapisha picha yake akiwa ameshikilia shada la maua, na kusema hilo ndilo tukio maalum la wiki yake.

"Mapenzi ni kitu kizuri," aliandika.

Mahusiano ya mwisho ya hadharani ya Betty Kyallo yalikuwa na wakili Nick Ndeda.

Wawili hao walipoachana, Betty alisema walikuwa na mitazamo tofauti ya masuala fulani ya kimaisha.

"Katika mahusiano, ni kuhusu kufahamiana. Ilifika mahali ambapo tulikuwa hatuna mwelekeo sawa upande na uhusiano."

Hivi majuzi Nick alisema anampeza mpenzi wake wa zamani, akimtaja kama mtu mzuri.

"Ninakosa mambo fulani fulani, sitasema uwongo. Nishati nzuri na yote," Nick alisema.