Brown Mauzo afichua mpenzi mpya baada ya kutengana na mwanasosholaiti Vera Sidika (+picha)

Mauzo alionyesha picha ya mwanamke asiyetambulishwa na kuambatanisha na emoji ya moyo inayoashiria mapenzi.

Muhtasari

•Mauzo amedokeza kuhusu mahusiano mapya siku chache tu baada ya kutangaza kuachana na mwanasosholaiti Vera Sidika.

•Vera pia ameonekana na mwanamume asiyejulika mwingine, ishara kwamba naye amesonga mbele na maisha yake tayari.

Image: INSTAGRAM// BROWN MAUZO

Mwimbaji Fredrick Mutinda almaarufu Brown Mauzo amedokeza kuhusu mahusiano mapya siku chache tu baada ya kutangaza kuachana na mwanasosholaiti Vera Sidika.

Siku ya Jumatano, mwanamuziki huyo mzaliwa wa pwani alichapisha picha ya mwanamke asiyetambulishwa na kuambatanisha na emoji ya moyo inayoashiria mapenzi.

Hata hivyo, hakushiriki maelezo zaidi kuhusu mwanamke huyo.

Haya yanajiri wiki chache tu baada ya mwanamuziki huyo kutangaza mwisho wa ndoa yake ya zaidi ya miaka miwili na mama wa watoto wake wawili, Vera Sidika.

Image: INSTAGRAM// BROWN MAUZO

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mauzo alitangaza kuwa yeye na Vera wamekubali kwenda njia tofauti kwa manufaa yao na ya watoto wao.

"Wapendwa marafiki na wafuasi, nilitaka kuchukua muda kushiriki habari za kibinafsi. Baada ya kufikiria sana, mimi na Vera Sidika tumeamua kuachana. Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti,” Mauzo alitangaza Jumatano.

"Safari yetu pamoja imejawa na nyakati zisizosahaulika, lakini tumefikia hatua ambayo ni bora kwa sisi na watoto wetu, Asia Brown na Ice Brown, kusonga mbele tofauti," Brown Mauzo alisema.

Alishukuru kila mtu ambaye amekuwa sehemu ya uhusiano wao ambao wamekuwa wakijivunia na kuuonyesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunataka kuwashukuru nyote kwa upendo wenu usioyumba na sapoti katika kipindi chote cha uhusiano wetu. Kutiwa moyo na nyinyi kumemaanisha ulimwengu kwetu. Tunapoanza sura hii mpya, tunaomba ufahamu wenu na heshima yenu kwa faragha yetu wakati huu,"

Aidha, alidokeza kuwa ukurasa  unaofuata wa maisha yao utakuwa kuhusu uponyaji wa moyo baada ya kuachana na kukumbatia yake yaliyo mbele.

"Ingawa sehemu zetu zinaweza kutofautiana, tutathamini kumbukumbu ambazo tumeunda pamoja. Sote tunasalia kushukuru kwa masomo tuliyojifunza na ukuzi ambao tumepitia. Lengo letu sasa ni uponyaji na kukumbatia siku zijazo kwa mioyo iliyo wazi. Asanteni kwa mara nyingine tena kwa kuwa sehemu ya safari yetu,” alisema.

Tangu kutangazwa kwa habari za kuachana kwao, Vera sidika amekuwa akifurahia muda nchini Marekani. Yeye pia ameonekana na mwanamume asiyejulikana mwenye miraba minne, ishara kwamba naye amesonga mbele na maisha yake tayari.