Diana Marua azungumzia Bahati kuwa mgonjwa siku yake ya kuzaliwa, kutotaka waisherehekee

Diana hata hivyo alikaidi na kumwandalia mumewe karamu ya kufana.

Muhtasari

•Wanandoa hao walikuwa na mipango mingine mikubwa ambayo ilikuwa inakuja na hivyo Bahati hakutaka wafanye karamu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

•Mama huyo wa watoto watatu alimsherehekea mumewe na kueleza jinsi anavyojivunia kuwa sehemu ya safari yake.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Diana Marua amefichua kwamba alipanga karamu ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya mume wake Bahati kinyume na matakwa yake.

Wanandoa hao walikuwa na mipango mingine mikubwa ambayo ilikuwa inakuja na hivyo Bahati hakutaka wafanye karamu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Diana hata hivyo alikaidi na kumwandalia mumewe karamu ya kufana.

"Singeruhusu siku hii ipite hivi hivi," Diana alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumanne.

Aliambatanisha ujumbe huo na video inayomuonyesha akimwagiza Bahati afunge macho yake kwa kitambaa kabla ya kumsurprise.

Kando na wao kuwa na mipango, Bahati  pia alikuwa mgonjwa na hivyo kuifanya siku yake maalum ionekane kuwa mbaya.

"Ulikuwa mgonjwa, ulitaka kulala tu na iliniumiza moyo kukuona unatimiza miaka 30 namna hiyo. Lakini, nilifanya nilichofanya na ninafuraha uliikumbatia na kumaliza mwenye nguvu," Diana Marua alisema.

Mama huyo wa watoto watatu alimsherehekea mumewe na kueleza jinsi anavyojivunia kuwa sehemu ya safari yake.

"Mwongo ni wa 3. Miaka 30 ya kukabili maisha na changamoto zake na kutoka kama BINGWA, daima! Ninajivunia kuwa sehemu ya safari yako ya maisha na kukuona ukisherehekea miaka 30 zaidi yangu hakika ni tunda kwenye keki ."

"NAKUPENDA, DAIMA. HERI YA KUZALIWA KWA MARA NYINGINE TENA MFALME WANGU. UNASTAHILI HII NA MENGINEYO  @BAHATIKENYA ❤️," alisema.

Bahati alisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Desemba 22, 2022 ambapo alitimiza umri wa miaka 30.

Wakati akisherehekea siku hiyo maalum  kwenye ukurasa wake wa Instagram, Bahati alisema ilikuwa siku yake kuu.

"Hatimaye, Bahati ako na miaka thelathini. Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa ya 30. Leo ni siku yangu kuu. Nilizaliwa 22 dec 1992," aliandika kwenye Intagram  siku ya Alhamisi, Desemba 23.

Baba huyo wa watoto wanne hata hivyo alifichua kwamba hakuweza kuandaa  karamu ya kusherehekea siku hiyo kwa vile alikuwa mgonjwa.

Wakati huo, Bahati alifichua kwamba alikuwa mgonjwa kwa muda wa takriban wiki moja ambayo ilikuwa imepita na alikuwa akitumia dawa.

"Natimiza miaka 30 leo lakini kwa bahati mbaya nimekuwa mgonjwa kwa wiki moja. Sasa ninatumia dawa, ilinibidi kuahirisha sherehe kutokana na dawa," Bahati alisema kwenye Instastori zake.

Hata hivyo alidokeza kuwa angeandaa karamu ya kusherehekea hatua mpya katika maisha yake mnamo Januari  28, 2023.

Wakati huo huo, mwimbaji huyo alimuomba mke wake Diana Marua kukubali waongoze mtoto mwingine mmoja wa mwisho.

"Situpate kamoja kengine ka mwisho tuu. Nimekuwa mgonjwa kwa kiwango cha chini kwa wiki moja sasa kwa hivyo ilinibidi kuahirisha sherehe yangu ya kuzaliwa, lakini habari Diana Marua, sijapoteza hamu," alisema.

Huku akimsherehekea mnamo siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake, Diana alimtaja mumewe kuwa mume wake, mfalme wake, mshirika wake wa maombi, nguvu zake, nguzo yake na baba wa watoto wake.

Ninakusherehekea kila siku lakini leo ni siku maalum kwa sababu ni siku yako ya kuzaliwa 🎉 KARIBU KWENYE GHOROFA YA TATU MPENZI @BAHATIKENYA ❤️," Diana Marua alimwandikia mumewe kwenye Instagram.

Aliongeza, "Zawadi kubwa zaidi ni kuwa nawe kila siku na kukuona katika 30 ukiwa mchangamfu, mwenye furaha na umetosheka. Huwa inanipa furaha na amani."

Mama huyo wa watoto watatu alimtakia Bahati furaha tele maishani, mafanikio mengi, baraka na neema ya Mungu.

Pia alimhakikishia kuhusu upendo wake mkubwa kwake na kumweleza jinsi huwa anamuombea mara nyingi.