Harmonize aonyesha mapenzi makubwa kwa Eve Mungai, mpenziwe ajibu "Hii imeenda!"

"Unaonekana mzuri sana usiku wa leo," alisema Harmonize.

Muhtasari

β€’Baada ya kuwasili, Konde Boy  alishiriki mahojiano na mtangazaji huyo ambapo alizungumzia masuala mbalimbali.

β€’Bosi huyo wa Kondegang pia aliendelea kuonyesha upendo kwa Eve chini ya video yake ambayo alichapisha kwenye Instagram.

Image: INSTAGRAM// EVE MUNGAI

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameonyesha upendo kwa mhoji maarufu wa Kenya, Eve Mungai.

Wawili hao walikutana siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi wakati alipowasili kwa ajili ya shoo yake kubwa mjini Embu ambayo ilifanyika usiku wa Jumamosi.

Baada ya kuwasili, Konde Boy  alishiriki mahojiano na mtangazaji huyo ambapo alizungumzia masuala mbalimbali.

"Niko hapa na mrembo Eve na tunaenda Embu usiku wa leo. Itakuwa wazimu. Ninaita kila mtu kujitokeza. Usikose hii," mwimbaji huyo alisema baada ya mahojiano.

Baada ya mahojiano, Eve aliungana na staa huyo wa Bongo kwa tamasha lake la usiku katika kilabu moja mjini Embu.

Mtangazaji huyo alipojitokeza kwenye jukwaa, Harmonize alishindwa kujizuia na kukiri jinsi alivyoonekana mzuri.

"Unaonekana mzuri sana usiku wa leo," alisema Harmonize.

Bosi huyo wa Kondegang pia aliendelea kuonyesha upendo kwa Eve chini ya video yake ambayo alichapisha kwenye Instagram.

"MALKIAπŸ‘Έβ€οΈ" Harmonize aliandika kwenye video ya Eve  akitembea kwa madaha.

Eve aliambatanisha video hiyo kwa wimbo wa Harmonize na Ibraah "One night stand"

Staa huyo wa Bongo pia alichora emoji za upendo chini ya video nyingine ya Eve ambayo alichapisha Jumapili. Eve kwa upande wake pia alijibu kwa emoji ya moyo ambayo kwa kawaida huashiria upendo.

Wanamitandao wamekuwa na maoni tofauti kuhusu shughuli za hivi majuzi za wawili hao huku wengine wakienda hadi kukisia kuwa kuna mahapa yanayojengwa kati yao.

Mpenzi wa Eve, Director Trevor ni miongoni mwa ambao wameweza kutoa maoni kuhusu matendo ya wawili hao.

"Hii imeenda πŸ˜‚πŸ˜‚ Harusi ni lini Mmakonde," alisema.

Wanamitandao wengine wengi walikubaliana na maoni ya Trevor huku makumi pia wakitoa maoni, "Hii imeenda"

Katika jibu lake, Eve alisema "Mtulie bana"