"Hii imeenda!" Samidoh aonywa baada ya mkewe kuonekana na mwanajeshi wa Marekani

Bi Edday Nderitu alionekana mwenye furaha sana akiwa amesimama kando na mwanajeshi huyo mzungu mrefu.

Muhtasari

•Edday, ambaye anafurahia likizo na watoto wake katika nchi hiyo ya Magharibi, alishiriki picha hiyo huku akiwasalimu mashabiki wake.

•Wengi wa wanamitandao waliotoa maoni walimhusisha Edday kimapenzi na mwanajeshi huyo huku baadhi wakimuonya mume wake Samidoh.

Samidoh, Edday Nderitu, na mwanajeshi wa Marekani
Image: HISANI

Siku ya Jumanne, mke wa mwimbaji Samidoh, Bi Edday Nderitu alichapisha picha yake akiwa na afisa wa jeshi la anga la Marekani.

Edday, ambaye anafurahia likizo na watoto wake katika nchi hiyo ya Magharibi, alishiriki picha hiyo huku akiwasalimu mashabiki wake.

"Usiku mwema kutoka upande huu wa dunia. Hakuna lingine ila maombi," alisema kwenye picha hiyo aliyochapisha kwenye  Facebook.

Pichani, mama huyo wa watoto watatu alionekana mwenye furaha sana akiwa amesimama kando na mwanajeshi huyo mzungu mrefu.

Mamia ya watumizi wa mtandao wa Facebook walimiminika chini ya chapisho hilo na kutoa maoni tofauti kuhusiana na picha aliyochapisha. Wengi wa wanamitandao waliotoa maoni walionekana kumhusisha Edday kimapenzi na mwanajeshi huyo huku baadhi wakionekana kumuonya mume wake Samidoh.

Tazama baadhi ya maoni ya wanamitandao:-

Nelly Precious: It has went this. I don't know why but am happy for this woman.

Lemiso Sato Emmanuel: The taste is permanent, Uniform.

Maggie Shii Ndehera Thayu: Hii imeenda

Sarah Daniels: It has went, btw change is always good. Congratulations. Samidoh amka kimeibiwo.

Kimberly Shelmith: Usitoke huko kama hujapata love of your life.

Baadhi ya wanamitandao walionekana wakimshauri mama huyo wa watoto watatu kumtema Samidoh na kubaki na mwanajeshi huyo.

Wengine walidai kuwa Edday ana ladha ya wanaume waliovalia sare kwani mbali na muziki, Samidoh pia ni afisa wa polisi.

Mwaka jana, mwimbaji huyo wa Mugithi ambaye ni afisa wa Polisi wa Utawala alisema hajapata sababu ya kuacha kazi ya polisi licha ya mafanikio yake katika tasnia ya muziki. Mara nyingi yeye hushiriki picha na video zake akitumbuiza katika sehemu mbalimbali za dunia lakini si akitoa huduma za afisa wa polisi.

"Ninafanya kazi siku za wiki na inapohitajika pamoja na kipindi cha wikendi huwa nafanya muziki wangu, kama talanta nyingine yoyote katika huduma ya polisi," alisema katika mahojiana na Word Is.

Msanii huyo alisema alijitahidi sana kupata kazi hiyo.

"Umewahi kwenda kwenye zoezi la kuajiri polisi na kuona watu wasio na mashati wakichukuliwa kupitia shughuli mbalimbali?" alisema.

"Kuacha kazi uliyotafuta chini ya mazingira hayo ni chungu sana."