Jinsi Zuchu alivyomsherehekea mpenziwe Diamond siku yake ya kuzaliwa

Msanii huyo alimtambua Diamond kama mtu maalum sana kwake na shujaa wake.

Muhtasari

•Zuchu alisema kuwa kila siku angependa kumkumbuka bosi huyo wake kama mtu Mcha Mungu sana.

•Bosi huyo wa WCB alisherehekea kutimiza miaka 32.

katika ziara yao ya Ufaransa.
Diamond Platnumza na anayedaiwa kuwa mpenziwe, Zuchu katika ziara yao ya Ufaransa.
Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Siku ya Jumapili, Oktoba 2, staa wa Bongo Diamond Platnumz aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa.

Bosi huyo wa WCB alisherehekea kutimiza miaka 32.

Watu wengi wakiwemo mashabiki, familia, marafiki wa karibu na wasanii wenzake walitumia siku hiyo kumsherehekea.

Msanii wake, Zuchu, ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa hakuachwa nyuma katika kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa. Alisema kuwa kila siku angependa kumkumbuka bosi huyo wake kama mtu Mcha Mungu sana.

"Biggy, ishi kwa muda mrefu. Chapisho la pili ni jinsi ninavyotaka kukukumbuka kila siku," aliandika kwenye Instagram.'

Zuchu aliambatanisha ujumbe wake na video iliyomuonyesha Diamond akifanya sala ndani ya chumba chake.

Video nyingine iliyofikia Radio Jambo ilimuonyesha binti huyo wa Malkia wa Mipasho Khadija Kopa akiwaomba mashabiki wake wamwimbie Diamond wimbo wa 'Happy Birthday' wakati akitumbuiza usiku wa kuamkia siku yake ya kuzaliwa.

Wakati huo alimtambua Diamond kama mtu maalum sana kwake na shujaa wake mkubwa.

"Yeye ni mtu maalum sana kwangu. Nitamtumia video hii. Nataka mnisaidie kumuimbia shujaa wangu 'Happy Birthday'. Yeye ni shujaa wangu. Yeye ndiye shujaa wangu pekee," alisema kabla ya kuongoza umati  kuimba wimbo 'Happy Birthday.'

Aliyekuwa msanii wa WCB Rayvanny pia alimtambua bosi wake wa zamani mnamo siku yake ya kuzaliwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny alimwandikia Diamond, "Maisha marefu simba!"

Hatua ya Rayvanny kumsherehekea Diamond inafutilia mbali tetesi kwamba wawili hao hawapo katika maelewano mazuri.