"Jiridhishe na DNA" Harmonize amtaka Ibraah amkubali mtoto anayedaiwa kuwa ni wake

Muhtasari

•Harmonize amemshauri msanii huyo wake kumkubali mtoto huyo pia huku akiahidi kusaidia katika malezi.

•Clyna alijitokeza kulalamika kuwa Ibraah ametelekeza jukumu la malezi ya mtoto wao na kumwagiza awajibike.

Image: INSTAGRAM// IBRAAH

Harmonize amekubaliana na maoni ya baadhi ya wanamitandao wengi kuwa mtoto anayedaiwa kufanana na Ibraah kwa kweli ni wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmonize amemshauri msanii huyo wake kumkubali mtoto huyo pia huku akiahidi kusaidia katika malezi.

"Brother tuletee huyu mfalme tutakopa, tutaiba, tutatapeli ili mradi mkono uende kinywani. Mungu na Masela haina kufeli !!" Harmonize aliandika kwenye Instastori zake.

Bosi huyo wa Kondegang aliendelea kumshauri  Ibraah achukue hatua ya kufanya DNA na mtoto huyo ili kutatua fumbo la kuhusika lililopo.

Ameonyesha kukubaliana na maoni kuwa mtoto huyo ana maumbile kama ya Ibraah na tayari amemkubali kuwa mjukuu wake.

"Ndenda tu, ukajiridhishe na DNA upate amani ya moyo ila huyu Chinga. Mjukuu wa mzee Kondeboy," Alisema.

Image: HISANI

Mtoto anayezungumziwa ametambulishwa kama Zein Ibrahim Nampunga na ni mwanawe mwanadada Clyna almaarufu Sugar.

Hivi majuzi Clyna alijitokeza kulalamika kuwa Ibraa ametelekeza jukumu la malezi ya mtoto huyo na kumwagiza awajibike. Alimshtumu mwanamuziki huyo kwa kuwa na 'utoto' mwingi huku akidai kuwa amekuwa akiogopa kuitwa baba.

"Labda ana utoto. Nimemzidi umri kwa mwaka mmoja. Nimezaliwa 97 yeye amezaliwa 98. Kitendo cha kuitwa baba amekuwa akikiogopa sana. Drama ni nyingi. Ibraah hamhudumii mtoto. Amekuwa mtu mgumu. Hata hivyo ananiheshimu sana," Mishepu alisema.

Clyna alisema kuwa yupo tayari kwa Ibraah kufanyia mtoto wake DNA ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye baba mzazi.

Katika kile kilichoonekana kuwa jibu lake kwa mwanadada huyo, Ibraah aliandika "Msinipe watoto wa watu mimi sina mtoto."