Kama singekuwa na mtoto ningekuwa nimekufa juu ya stress- Kartelo azungumzia uzazi

Kartelo alifichua kuwa mpango wake ni kupata watoto zaidi ya saba.

Muhtasari

•Kartelo alifichua kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na mwanawe ambao unafanya afurahie sana kukaa naye.

•Mchekeshaji huyo alidokeza kuwa bado hajafunga ukurasa wa kupata watoto zaidi ya mmoja aliye naye.

Image: INSTAGRAM// KARTELO

Mchekeshaji Nickson Chege almaarufu Kartelo amekiri kwamba hali ya kuwa baba imemtia moyo sana.

Katika mahojiano na Eve Mungai, baba huyo wa mtoto wa miaka miwili alisema anafurahia sana hali ya  kuwa mzazi mdogo na kubainisha  kuwa mwanawe ni chanzo cha furaha kubwa kwake.

Kartelo alifichua kuwa kuna uhusiano mzuri kati yake na bintiye ambao unafanya afurahie sana kukaa naye.

"Inanipeleka poa sana. Inanibamba. Mimi kama singekuwa na mtoto sijui ningekuwa nimekufa na stress. ,Mtoto hunisaidia kwa sababu mimi nikiingia kwa nyumba kwanza huwa ananitoa stress, huwa tunacheza na yeye hapo ananibamba. Ata ninaweza kukosa kufanya chochote kingine kwa hii duniia niwe nashinda tu kwa nyumba na mtoto wangu," Kartelo alisema.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 24 alibainisha kuwa bintiye sio mtoto wake tu bali pia ni rafiki wake mkubwa.

Alisema hatua ya kuwa mzazi limbadilishia maisha kwa kuwa ilimpa masomo mengi ya kimaisha ambayo hakuwa nayo.

"Kuna vitu mingi sikuwa najua. Ukishakuwa baba ndio sasa unaanza kuzijua. Vitu kama kuwajibika, kuwa na subira na mengi. Hiyo safari ya kuona mtoto akikua imenifunza sana kuhusu maisha," Alisema.

Kartelo pia alisema kuwa baba kulifanya apate motisha wa kutia bidii zaidi katika kazi zake za usanii.

"Mwaka ujao mwanangu anaingia chekechea. Nimeskia wazazi wakisema siku hizi kuingiza mtoto shule ni ngorI. Nataka hadi mimi niwe nimejipanga,"

Aidha, mchekeshaji huyo alidokeza kuwa bado hajafunga ukurasa wa kupata watoto zaidi ya mmoja aliye naye.

Alifichua kuwa mpango wake ni kupata watoto zaidi ya saba.

"Nataka nipate chini zaidi watoto saba. Mama ni Waria, hiyo pande hawachezangi. Wanaweza kupatia hadi 12 na hawahemi. Hiyo pande niko sawa," Alisema.

Kartelo alieleza kwamba sababu yake kutoonyesha mpenziwe hadharani ni kwa kuwa yeye hapendi umaarufu.