"Kwani nitakosa pesa!" Dadake Diamond, Esma Platnumz avunja kimya baada ya Zuchu kum-unfollow

Muhtasari

•Zuchu alichukua hatua ya kuacha kumfuatilia dada huyo wa bosi wake siku chache zilizopita kwa sababu ambazo hakuziweka wazi.

•Esma alisema hajawahi kuwa na urafiki wa karibu na Zuchu.

Image: INSTAGRAM// ESMA PLATNUMZ NA ZUCHU

Malkia wa Bongo Zuhura Othman almaarufu Zuchu hamfuatili tena dada yake Diamond, Esma Platnumz.

Zuchu alichukua hatua ya kuacha kumfuatilia dada huyo wa bosi wake siku chache zilizopita kwa sababu ambazo hakuziweka wazi.

Esma akiwa katika mazungumzo ya simu na Juma Lokole hata hivyo aliweka wazi  kuwa hatua ya mwanamuziki huyo haikumshangaza.

"Cha ajabu kipi sasa? Nablockiwa na mawifi, itakuwa wafanyakazi wa WCB wakiniblock!" Esma alisema.

Mfanyibiashara huyo alibainisha kuwa hatua ya Zuchu kuacha kumfuatilia haimpunguzii chochote.

"Umesikia ati akiacha kuniunfollow nitakosa pesa?" Alisema.

Esma alisema mara yake ya mwisho kukutana na Zuchu ni wakati ambapo walipomtembelea Mama Dangote hospitalini mapema mwezi huu.

Alisema hajawahi kuwa na urafiki wa karibu na mwanamuziki huyo. Hata hivyo aliweka wazi kuwa hafahamu ugomvi wowote kati yao.

"Mimi na Zuchu hata hatuna ukaribu naye. Msanii ambaye niko na ukaribu sana ni Mbosso," Alisema.

Aidha, Esma alibainisha kwamba hajakuwa kwenye mtandao wa Instagram sana katika siku za hivi majuzi.

Licha ya yaliyojiri hivi majuzi, tumeweza kubaini kuwa Zuchu bado anamfuatilia malkia huyo wa muziki wa Bongo. 

"Niko bize natafuta pesa. Siku hizi ata siangalii akaunti za watu. Ata akaunti ya Mama Dangote sijui niliangalia lini mwisho. Niko bize," Alisema.

Haya yanajiri takriban wiki mbili tu baada ya mama huyo watoto wawili kusema huwa anatia bidii kazini ili kutajirika kama nduguye.

Akiwa kwenye mahojiano na Global TV, Esma alisema wivu wake kwa utajiri wa Diamond ndio unaomfanya ajitume zaidi katika biashara yake ya nguo.

"Mimi natamani niwe kama Naseeb. Sio eti niwe mwanamuziki lakini natamani yale maendeleo yake. Ili niwe kama yeye ni kujituma kwa bidii," Esma alisema.

Mfanyibiashara huyo aliweka wazi kuwa kamwe hawezi kujibweteka eti kwa kuwa kaka yake ni tajiri mkubwa.

Alisema hawezi kufikiria kutegemea utajiri wa Diamond maishani kwa kuwa ni jambo ambalo linaweza kumletea dharau.