Mahaba hewani huku Juliani na Lilian Nganga wakisherehekea penzi lao nzito

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili sasa na tayari wana mtoto wa mwaka mmoja.

Muhtasari

•Walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuonyesha jinsi uhusiano wao ulivyoimarika na jinsi walivyo na furaha pamoja.

•Walihalalisha muungano wao kwa kufunga pingu za maisha mapema mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa muda.

Lilian Nganga na mume wake Juliani
Image: INSTAGRAM// LILIAN NGANGA

Siku ya Jumatatu, wanandoa maarufu wa Kenya Lilian Nganga na mwimbaji Julius Owino almaarufu Juliani waliwakumbusha wanamitandao kuhusu mapenzi yao mazito kwa kushiriki picha zao nzuri wakiwa pamoja.

Wawili hao ambao ni wazazi wa mvulana wa mwaka mmoja walitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuonyesha jinsi uhusiano wao ulivyoimarika na jinsi walivyo na furaha pamoja.

“Jana<<< 🎶playback 🎶 @julianikenya,” Lilian Nganga aliandika kwenye picha nzuri yake na mumewe aliyoichapisha kwenye Instagram.

Katika picha hiyo ambayo Juliani pia aliiweka kwenye ukurasa wake, wawili hao walionekana kuwa na furaha sana pamoja na tabasamu kubwa za kupendeza ziliandikwa kwenye nyuso zao.

 Juliani pia alishare picha nyingine yake akiwa na mama huyo wa mtoto wake wakiwa katika sehemu ambayo ilionekana kama eneo la burudani.

Image: INSTAGRAM// JULIANI

Wawili hao wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili sasa na tayari wana mtoto wa mwaka mmoja pamoja. Walihalalisha muungano wao kwa kufunga pingu za maisha mapema mwaka jana baada ya kuchumbiana kwa muda.

Walifunga ndoa katika hafla ya siri ya iliyofanyika jijini Nairobi mwezi Februari mwaka jana, mnamo siku ya kuzaliwa ya Lilian Nganga .

Picha za harusi yao hazikusambaa sana kwani picha moja tu ndiyo iliyoweza kupenyeza kwenye mitandao ya kijamii. Lilian alikuwa amevalia gauni la rangi ya waridi lililokuwa limebubujika hadi chini na mume wake Juliani alikuwa amevalia shati nyeupe-theluji na koti ya pembe, suruali nyeusi  na viatu vyeupe.

Juliani alikuwa na wasimamizi watatu, huku Ng’ang’a akiwa na wasimamizi wawili wa kike waliovalia gauni ]la kupendeza.

Mandhari ya harusi hiyo yalikuwa rangi nyeupe na nyeusi na wanandoa hao waliweza kuwaalika watu chini ya 50.

Akizungumza na Mpasho mwaka jana, Lilian Nganga alisema kuwa harusi hiyo ilikuwa ya kipekee na ya faragha.

Hakukuwa na mengi ya kupanga kwa hivyo haikutuchukua muda kupanga harusi hiyo, ilichukua muda wa miezi miwili pekee,”alisema.

Wawili hao waliweka mahusiano yao bayana mwezi Septemba, mwaka wa 2021 walipojitokeza  kutangaza kuwa wanachumbiana.