Mama na dada yake Diamond wastaajabu haogopi nyoka, atuhumiwa kwa Ushetani

Baadhi ya wanamitandao walimshutumu Diamond kwa kujihusisha na Ushetani.

Muhtasari

•Mwanamuziki huyo mahiri mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

•Esma Platnumz alishangazwa na jinsi alivyomshika mnyama huyo kwa ujasiri ilhali anawaogopa paka na mbwa.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Siku ya Ijumaa, staa wa Bongo Diamond Platnumz alitangaza kwamba yeye ni mmiliki mpya wa mnyama aina ya nyoka.

Katika tangazo lake kwenye Instagram, mwanamuziki huyo alibainisha kuwa siku zote kumiliki nyoka kipenzi imekuwa ndoto yake.

Mwanamuziki huyo mahiri mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

"Siku zote nimekuwa na shauku ya kuwa na nyoka wangu kama kipenzi ❤️🐍.. jameni kukutaneni na rafiki yangu mpya," alitangaza siku ya Ijumaa.

Mwimbaji huyo anayetambuliwa kote duniani alifichua kwamba nyoka huyo wake atatambuliwa kwa jina  Chichi.

Diamond aliambatanisha tangazo lake na video iliyomuonyesha akicheza na mnyama huyo anayeteleza huku kundi kubwa la watu wakiwa wamemzunguka.

Katika video hiyo, mwimbaji huyo alisikika akikiri upendo wake mkubwa kwa nyoka na kueleza furaha yake kwa kumpata wa kufuga nyumbani

"Huyu mimi namfuga mnyama huyu nyumbani. Mimi napenda nyoka sana," alisika akisema.

Umati mkubwa ulitazama kwa udadisi alipokuwa akichezea na nyoka huyo kwa usaidizi wa mwanamke aliyekuwa akimuonyesha jinsi ya kumshika. Hakuonesha uoga wowote na badala yake alionekana kufurahi sana kumshika.

Mamia ya wanamitandao wakiwemo wanafamilia, watu wa karibu na watu wengine mashuhuri walifurika chini ya chapisho hilo na kutoa maoni tofauti kuhusu hatua yake ya kumiliki mnyama huyo anayeogopwa na wengi.

Dada yake Esma Platnumz alishangazwa na jinsi alivyomshika mnyama huyo kwa ujasiri ilhali anawaogopa paka na mbwa.

"Ajabu ni kwamba nyoka hamuogopi, mbwa na paka ndio anaogopa. @officialzuchu yule paka wetu tumletee na sie," Esma aliandika.

Chini ya maoni ya Esma, Mama Dangote alisema, "Maajabu sana"

Wanamitandao wengine wengi kwenye sehemu ya maoni pia walishangazwa na jinsi bosi huyo wa WCB alivyomshika mnyama bila woga. Baadhi hata hivyo walimshutumu kwa kujihusisha na Ushetani kwani jamii nyingi za Kiafrika mara nyingi humhusisha nyoka na nguvu za giza.

@charlotteakankunda Asante kwa kubainisha kuhusu wewe kuwa wa Illuminati

@_cheusi Usituchore bana, uchawi tu

@kesh250 Wenye chuki watasema hiyo ni ishara ya Illuminati

@_kasarani_finest Watu sio wajinga bana hiyo ndiyo itaongeza utajiri na umaarufu wako

@officialsammy_cool Sasa ndio tumejua kumbe una uchawi ndani ya mafanikio yako