logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mambo ni kortini sasa! Mulamwah kumshtaki Carrol Sonie, aibua madai mazito dhidi yake

Mulamwah ametishia kumshtaki mzazi mwenzake Carrol Sonie huku drama kati ya wapenzi hao wawili wa zamani ikiendelea.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani06 February 2024 - 12:36

Muhtasari


  • •Mulamwah ametishia kumshtaki mzazi mwenzake Caroline Muthoni Ng’ethe huku drama kati ya wapenzi hao wawili wa zamani ikiendelea.
  • •Mulamwah alamika kuhusu video ya hivi majuzi ambayo Sonie ambapo inadaiwa alimsingizia kuwa amepuuza majukumu yake ya malezi ya mtoto. 

Mchekeshaji mashuhuri wa Kenya David Oyando almaarufu Mulamwah ametishia kumshtaki mzazi mwenzake Caroline Muthoni Ng’ethe huku drama kati ya wapenzi hao wawili wa zamani ikiendelea.

Katika taarifa yake siku ya Jumanne, baba huyo wa binti mmoja alibainisha kuwa amefanya uamuzi wa kuchukua hatua za kisheria baada ya juhudi za kutatua masuala yao kwa njia ya kidiplomasia kushindwa.

Mulamwaha alishiriki barua ndefu iliyoandikwa na mawakili wake kwa mpenzi huyo wake wa zamani akieleza kutoridhika kwake na jinsi Sonie amedaiwa kupuuza barua ya awali na jinsi ambavyo amedaiwa kuendelea kuibua madai ya uwongo dhidi yake.

"Umeendelea kumchafulia jina mteja wetu bila sababu huku ukimnyima haki ya kumuona mtoto," barua hiyo iliyotiwa saini na MNO Advocates LLP ilisoma.

Katika barua hiyo, Mulamwah aliendelea kulalamika kuhusu video ya hivi majuzi ambayo mpenzi huyo wake wa zamani aliifanya kwenye YouTube ambapo inadaiwa alimsingizia kuwa amepuuza majukumu yake ya malezi ya mtoto. 

"Ulizua maoni ya uwongo kwamba mteja wetu amekataa na/au amepuuza kushiriki gharama ya kumlea mtoto. Hii ni licha ya kukiri kwako kwamba mara kadhaa mteja wetu amekutumia pesa kupitia MPESA kwa ajili ya matunzo ambayo umeghairi bila kutoa sababu,” barua hiyo ilisoma.

Mchekeshaji huyo pia alilalamika kuhusu muigizaji huyo kuondoa jina lake kwenye cheti cha kuzaliwa cha binti yao.

Aidha, alitumia fursa hiyo kutangaza nia yake ya kumshirikisha mpenzi huyo wake wa zamani katika majadiliano yanayohusiana na malezi ya msichana wao wa miaka miwili.

Kufuatia malalamiko yote aliyotoa, Mulamwah aliendelea kutoa madai matatu makuu kwa mama huyo wa bintiye.

Madai hayo ni pamoja na;

i) Kufuta taarifa za kumchafulia jina na kuomba msamaha hadharani.

ii) Kufuta picha na video zote za mtoto kwenye chaneli yake ya YouTube.

iii) Kushiriki stakabadhi ya cheti cha sasa cha kuzaliwa cha mtoto wao na sababu ya kubadilisha jina lake bila ridhaa yake.

"Tafadhali kumbuka kuwa mteja wetu yuko tayari kukupa siku 10 kuanzia tarehe ya kupokea barua hii ili kutii kama ilivyoelezwa hapo juu," ilisoma taarifa iliyoandikwa Februari 1, 2024.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved