KHERI ZA SIKU YA KUZALIWA MASSAWE!

Massawe Japanni asherehekea kutimiza miaka 40

Massawe amemshukuru Mola kwa miaka 40 ambayo ameishi na kwa yote aliyotimiza katika kipindi hicho.

Muhtasari

•Miongo minne imetimia sasa tangu malkia huyo wa matangazo kwa lugha ya Kiswahili alipotua humu duniani.

•Massawe anasherehekea siku yake ya kuzaliwa nchini Italia ambako anafurahia likizo yake ya siku kadhaa.

katika studio za Radio Jambo
Mtangazaji Massawe Japanni katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mtangazaji wa kipindi  cha Bustani la Massawe kwenye Radio Jambo, Massawe Japanni anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo, Julai 27.

Miongo minne imetimia sasa tangu malkia huyo wa matangazo kwa lugha ya Kiswahili alipotua humu duniani.

Huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Massawe amemshukuru Mola kwa miaka 40 ambayo ameishi na kwa yote aliyotimiza katika kipindi hicho.

"40. Wow! Ni hatua muhimu iliyoje! Naweza kusema tu, Asante Mungu! Kila mwaka umekuwa somo, fursa na wakati mwingine hasara. Muhimu zaidi, kila mwaka umekuwa baraka. Asante kwa kuwa sehemu ya safari yangu," Massawe alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha zake nzuri kadhaa zinazoonyesha wazi  jinsi anavyozidi kung'aa kadri miaka inavyosonga.

"Na sasa, kwa  adventure zaidi inayoitwa maisha," Alisherehekea.

Mtangazaji huyo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa nchini Italia ambako anaendelea kufurahia likizo ya siku kadhaa.

Mamia ya mashabiki wake, marafiki na watu wengine wa karibu wameendelea kumuandikia jumbe nzuri za kheri za siku ya kuzaliwa.

@isaiahlangat Happy 40th Birthday MJ

@_naomnyaboke Happy birthday sweetheart❤❤❤

@zkananu  Happy blessed birthday love❤❤

@bryoshavin Happy birthday

@valentineludiema Happy Birthday @massawejapanni😍😍

Katika kipindi cha miongo minne ambacho kimepita Massawe ameweza kutimiza mengi na kugusa nafsi za wengi.

Kwa sasa yeye ni mmoja wa watangazaji wanaoshabikiwa zaidi hapa nchini Kenya na hata nje ya mipaka. Ustadi wake mkubwa katika utangazaji umeweza kumpa jina la 'Queen of Swahili Radio.' 

Kando na utangazaji, Massawe pia ni mtu wa familia na ni kielelezo kwa wazazi wengi hasa walio na watoto wa kike. Yeye ni mzazi wa mabinti watatu.