Mbosso ni mwanaume wa aina gani katika mahusiano? - Baby mama wake afunguka

Staa huyo wa Bongo anapenda sana kudekezwa na kubembelezwa na mpenzi wake.

Muhtasari

•Rukia alifichua kuwa staa huyo wa anamthamini mpenzi mkweli, asiye na marafiki wengi na anayewekeza muda na mtoto wake.

•Rukia alifichua kuwa mwandani huyo wa Diamond Platnumz hupata ndoto za kiajabu mara nyingi akiwa usingizini.

•Pia alifichua kuwa kwa kawaida Mbosso hukasirika kwa urahisi  lakini baadae hutulia haraka sana.

Image: INSTAGRAM// MBOSSO

Mmoja wa wazazi wenza wengi wa Mbosso, Rukia Rucky almaarufu Mama Ikram amefunguka kuhusu kipindi cha mahusiano yake na msanii huyo.

Mbosso na Rukia walichumbiana takriban miaka mitatu iliyopita na wakajaliwa mtoto wa kiume mnamo Agosti 2019.  

Rukia amefichua kuwa msanii huyo wa WCB alimnyemelea na kumtongoza kupitia mtandao wa snapchat.

"Baba Ikram alianza kunitext snapchap. Tumeseji tukaanza urafiki kidogo baadae ndo tukaanza kuwa na mahusiano," Mama Ikram alisema katika mahojiano na Wasafi Media.

Kipusa huyo ndiye mpenzi wa mwisho wa Mbosso anayejulikana wazi.

Rukia alifichua kuwa staa huyo wa anamthamini mpenzi mkweli, asiye na marafiki wengi na anayewekeza muda na mtoto wake.

"Ni baba anayependa muda wote uwe na mtoto wake, anapenda sana mtoto wake, Hata anaweza asiwe na shughuli na wewe  kama hushughuliki na mtoto wake," Alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja alifichua kuwa kwa kawaida Mbosso hukasirika kwa urahisi  lakini baadae hutulia haraka sana.

"Ni mtu ambaye anapenda kusikiliza maneno ya watu, akiambiwa kitu kidogo anapatwa na wasiwasi,"

Alieleza kuwa msanii huyo hukasirika wakati mwenzake anapokosa kushika simu ama kutokuwepo nyumbani anapotembelea mwanawe.

Pia alifichua kuwa staa huyo wa Bongo anapenda sana kudekezwa na kubembelezwa na mpenzi wake.

"Mimi ni mtu ambaye napenda kujishusha, nikikosea naomba msamaha. Nilikuwa nikiomba msamaha, anapenda sana kubembelezwa. Sasa nikikosea nambembeleza bembeleza, 'Mbosso nisamehe'.." Alisema.

Rukia alifichua kuwa mwandani huyo wa Diamond Platnumz hupata ndoto za kiajabu mara nyingi akiwa usingizini.

Pia alifichua kuwa mzazi huyo mwenzake anapenda sana  kupikiwa ubwabwa kwa maharage au samaki. 

"Ukimpikia ugali usiku anakwambia huwa anaota ndoto mbaya akikula. Ata mchana labda awe na hamu na huo ugali ndio akule. Anapenda tu ubwabwa," Alisema.

Ingawa idadi halisi ya wanawake ambao amewahi kupata watoto nao haijulikani, Mbosso kwa kawaida huwa hafichi ukweli kuwa yeye ni baba wa watoto wengi.

Hata hivyo ameonekana kumpendelea zaidi  Rukia na ambaye ni mama ya mtoto wake wa mwiisho anayejulikana, Ikram. 

Hivi majuzi mwanamuziki huyo akiwa kwenye mahojiano alidokeza kuwa bado ana hisia kubwa kwa Rukia.

"Nafasi ya Mama Ikram katika moyo wangu ni kubwa sana kwa sababu kipindi nilikuwa naanza sanaa alikuwa ananisapoti sana. Mama Ikram ni special," Alisema katika mahojiano.

Aliongeza kuwa mtoto ambaye alipata na Bi. Rukia ni ,"Mwanangu wa dhahabu."