Milly Wajesus afunguka kuhusu binti ya mumewe Kabi na binamu yake kumtambua kama mamake

Kabi alikiri kupata mtoto na mmoja wa binamu zake takriban mwongo mmoja uliopita.

Muhtasari

•Ndanu alitaka kujua kuhusu uhusiano uliopo baina ya Milly na Abby Wajesus, ambaye ni binti ya mume wake, Kabi Wajesus na mmoja wa binamu zake.

•Baadaye Milly alidokeza kwamba hakutaka kuzungumza kuhusu suala hilo kwa kuwa ni la kihisia sana.

•Milly alisema haikuwa ngumu sana kumkubali Abby katika familia yake kwa kuwa amekua pamoja na watu wasio wa damu yake.

Milly Wajesus, Kabi na Abby Wajesus
Image: HISANI

Vipindi vipya vya kusisimua vya shoo ya Oh Sister! inayohusisha baadhi ya mastaa wanawakewa Kenya  vinaendelea kuonyeshwa kwenye Maisha Magic East kila Ijumaa.

Katika kipindi kilichoonyeshwa Ijumaa, Aprili 21, mwanavlogu Milliicent Wambui almaarufu Milly Wajesus alishiriki kikao na mjasiriamali Priscilla Ndanu Maina ambapo wawili hao walizungumza kuhusu masuala mbalimbali.

Wawili hao walizungumza kuhusu jinsi mabinti wa mhusika mwenzao kwenye shoo hiyo, Nicah The Queen walivyoonyesha ukali.

"Siwezi kuamini ukweli kuwa Slaver  alienda kuona watoto. Kwa hakika, watoto wa Nicah ni wakali. Wanajilinda sana. Ni wadogo lakini wanajua wanachotaka.Wao ni kama msichana wa kawaida ," Ndanu alimwambia Milly.

Milly alikubaliana na maoni ya mjasiriamali huyo na kubainisha kuwa siku hizi wazazi wanalea watoto kama hao.

Wakati wakiendelea na mazungumzo hayo, Ndanu alimshambulia mama huyo wa watoto wawili na swali gumu ambalo lilionekana kumshtua. Mjasiriamali huyo alitaka kujua kuhusu uhusiano uliopo baina ya Milly na Abby Wajesus, ambaye ni binti ya mume wake, Kabi Wajesus na mmoja wa binamu zake.

"Tukizungumza kuhusu wasichana, mtoto wa Kabi siku hizi ashaanza kukuita mama?" Ndanu aliuliza kwa ujasiri.

Milly ambaye wakati huo alikuwa akinywa kahawa aliweka kikombe chake chini  polepole huku mshtuko mkubwa ukiwa umechorwa usoni mwake. Alionekana kushtushwa sana na kukerwa na swali hilo na akawa ameduwaa.

Baadaye alidokeza kwamba hakutaka kuzungumza kuhusu suala hilo kwa kuwa ni la kihisia sana.

"Sitaki kulia!" alisema.

Takriban mwaka mmoja unusu, mama huyo wa watoto watatu aliweka wazi  tayari amemkubali Abby kuwa sehemu ya familia yake.

Kwenye mahojiano na SPM Buzz, Milly alisema anamchukulia Abby kama bintiye kwa sababu ndoa ilimuunganisha pamoja na Kabi.

"Abby ni kama binti yangu. Maadamu yeye ni damu ya mume wangu, yeye ni damu yangu pia. Hii ni kwa sababu tulipokuja pamoja tulifanywa kitu kimoja. Naamini hivo" Milly alisema.

Milly alisema haikuwa ngumu sana kumkubali Abby katika familia yake kwa kuwa amekua pamoja na watu wasio wa damu yake.

Kabi alishambuliwa sana mitandaoni mwaka wa 2021 baada ya kukiri kuwa ndiye baba mzazi wa Abby ingawa hapo awali alikuwa amekana madai hayo.