Mimi na Diamond tunaelewana zaidi sasa, tuko marafiki zaidi ya tulivyokuwa wapenzi- Zari Hassan

Zari alibainisha kuwa kuelewana kuzuri kwake na Diamond kumerahisisha ushirikiano wao katika malezi.

Muhtasari

•Zari alifichua kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakijadiliana mara kwa mara kuhusu njia bora ya kuwalea watoto wao.

•Zari alidokeza kuwa uhusiano wake na Diamond sasa umekuwa mkubwa zaidi ya wakati walipokuwa kwenye mahusiano.

Zari Hassan na Diamond Platnumz
Zari Hassan na Diamond Platnumz
Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE

Mwanasoshalaiti maarufu Zari Hassan ameweka wazi kuwa anashirikiana vizuri na  aliyekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz katika malezi ya watoto wao wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Katika mahojiano na Wasafi Media, Zari alifichua kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakijadiliana mara kwa mara kuhusu njia bora ya kuwalea watoto wao.

"Tumefanya malezi ya kushirikiana kuwa rahisi sana. Tumekuja pamoja na kusema tunataka bora zaidi kwa watoto wetu,tunaketi na kuongea," Zari alisema.

"Tuna maslahi yao bora moyoni; wanataka nini?  wanataka kuenda wapi? wanajiona wapi?"

Zari alikuwa akizungumza wakati wa karamu kubwa iliyoandaliwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya bintiye Tiffah Dangote.

Mama huyo wa watoto watano alibainisha kuwa kuelewana kuzuri kwake na staa huyo wa Bongo kumerahisisha ushirikiano wao katika malezi.

Alidokeza kuwa uhusiano wake na Diamond sasa umekuwa mkubwa zaidi ya wakati ambapo walikuwa kwenye mahusiano.

"Nadhani imekuwa rahisi kwa sababu sasa tunaelewana zaidi, sio kama wapenzi lakini tunaelewana kama wazazi na marafiki. Mimi na Diamond kwa sasa hivi tumekuwa marafiki zaidi ya jinsi tulivyokuwa wapenzi. Inafanya mambo kuwa rahisi kwetu," Alisema.

Zari na Diamond walitengana mwaka wa 2018 baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka minne.

Licha ya kutengana kwao, wawili hao wameendelea kushirikiana vizuri katika malezi ya watoto wao wawili. Diamond ameonekana mara nyingi akifanya ziara za kuenda Afrika Kusini kuwatembelea wanawe.

Wikendi, bosi huyo wa WCB na familia yake walijumuika na familia ya Zari kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Tiffah. 

Tiffah ambaye alitimiza miaka saba mnamo Agosti 6 pia aliandamana na babake wakati alipozuru Kenya kwa ajili ya kutumbuiza katika mkutano wa Azimio