Mke wa Samidoh amsihi ailinde ndoa yao kufuatia drama yao na Karen Nyamu

Edday amemsihi Samidoh azibe njia zote ambazo shetani anaweza kutumia kuharibu ndoa yao.

Muhtasari

•Edday alichapisha picha akiwa na baba huyo wa watoto wake, wakiimba wimbo 'Ihua ria Ngoro' (Ua la Moyo) wake Shifta Wa Maria.

•Karen Nyamu baadaye alitangaza kuwa amemaliza rasmi uhusiano wake na mwimbaji huyo mashuhuri.

Image: INSTAGRAM// EDDAY NDERITU, KAREN NYAMU

Edday Nderitu, mke wa mwimbaji wa Mugiithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh, amemsihi azibe njia zote ambazo shetani anaweza kutumia kuharibu ndoa yao.

Edday, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alichapisha picha akiwa na baba huyo wa watoto wake, wakiimba wimbo 'Ihua ria Ngoro' (Ua la Moyo) wake Shifta Wa Maria.

Wimbo huo unahusu mume kumwonyesha upendo mkewe. Unazungumzia uhakikisho na umuhimu wa kubaki imara kama wanandoa na kujenga tunda la upendo.

"Upendo huu una maadui wengi sana lakini kwa Mungu, nguvu za shetani hazina nguvu. Mpenzi wangu, tunatakiwa kuziba mashimo yote na kulinda upendo huu."

Ujumbe wa Edday kwa mumewe ulikuja saa chache baada ya kizaazaa kutokea wakati alipokabiliana na baby mama wake ambaye aliteuliwa kuwa Seneta, Karen Nyamu, jijini Dubai, Ijumaa usiku.

Karen Nyamu, ambaye ana watoto wawili na Samidoh na Edday nusura wapigane wakati wa shoo yake ya Mugiithi jijini Dubai.

Kufuatia hilo, Karen Nyamu baadaye alitangaza kuwa amemaliza rasmi uhusiano wake na mwimbaji huyo mashuhuri.

Alisema alitangaza kuachana hadharani kwa kuwa uhusiano wao ulikuwa hadharani.

"Najua ningeweza kumpigia simu na kumaliza kimya kimya lakini niliamua kuweka hadharani kama mchezo wa kuigiza na ugomvi umekuwa."

Karen Nyamu anadaiwa kuwa anatarajia mtoto wake wa nne.

Katika machapisho mbalimbali amethibitisha madai hayo.

Karen alimweleza shabiki mmoja aliyekuwa na shauku ya kutaka kujua kwamba aliona dalili za ujauzito wake kuwa tayari alikuwa amewatayarisha mashabiki wake kuhusu kupata mimba tena.

"Hutanilaumu kwani nilishasema nitarudi hivi karibuni."

Utafsiri: Samuel Maina