"Mnikome!" Huddah alalamikia kutongozwa na wanaume Watanzania wakiomba kumtunga mimba

"Nina wanaume wengi sana ndio maana nimechanganyikiwa. Sijui nimpe nani awe baba mtoto," alisema

Muhtasari

•Huddah alifichua kuwa kuna wanaume wengi watanzania ambao wanamtumia jumbe wakiomba kumtunga ujauzito.

•"Mnikome na hizo maDM zenu. Nina wanaume. Sijakosa wanaume.Wanaume hawakosekani, wako kila mahali," alisema.

Huddah Monroe

Mwanasosholaiti wa mashuhuri wa Kenya Huddah Monroe amewataka wanaume wa Tanzania kukoma kumtongoza kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwenye video aliyochapisha siku ya Jumatano, mrembo huyo mzaliwa wa Nairobi alifichua kwamba kuna wanaume wengi wa Kitanzania ambao wamekuwa wakimtumia jumbe kwenye Instagram wakiomba kumtunga ujauzito.

Huddah hata hivyo aliweka wazi kuwa hatafuti mwanaume wa kuwa baba wa mtoto wake kwani tayari ana wanaume wengi.

"Nina wanaume wengi sana ndio maana nimechanganyikiwa. Sijui nitampa nani ndio awe baba ya mtoto," alisema kwenye video.

Alisema kuwa atawafahamisha wafuasi wake wakati ambapo hatimaye ataamua mwanamume ambaye atazaa naye.

"Mnikome na hizo maDM zenu. Nina wanaume. Sijakosa wanaume.Wanaume hawakosekani, wako kila mahali," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo aliambatanisha ujumbe wake na screenshot kadhaa za jumbe ambazo alipokea kutoka kwa wanaume. Katika jumbe nyingi alizofichua, Watanzania walikuwa wakijitolea kumpa ujauzito.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya mwanasoshalaiti huyo kulazimika kujitokeza kufafanua madai yake ya ujauzito. 

Katika taarifa yake fupi siku ya Jumatatu, mfanyibiashara huyo wa vipondozi alidai kwamba ana ujauzito wa miezi mitatu.

"Ujauzito wa miezi mitatu," aliandika kwenye Instagram.

Siku moja baadaye hata hivyo, alijitokeza tena kupinga madai yake ya awali kuwa anatarajia mtoto wake wa kwanza.

"Nyie, mimi sio mjamzito," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo alieleza kwamba tumbo lake limeendelea kuwa kubwa na hivyo kufanya aonekane mjamzito.

Wakati huohuo, alidokeza kuwa hana mpango wa kupata mtoto hivi karibuni.

"Niko kwenye awamu yangu ya kuwa mwanamke mzima, tulieni. Hakuna mbegu ya kiume yenye nguvu ya kutosha kushika mayai yangu," alisema.

Kwa muda mrefu, mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Nairobi amekuwa akiweka mahusiano yake kuwa siri. Ni mara chache tu ambapo ameonekana akizungumza kuhusu mpenzi wake lakini mara kadhaa ameonyesha kumpenda sana mwanamume huyo ambaye bado hajajulikana hadharani.

Mwaka jana, alidaiwa kutoka kimapenzi na mwimbaji wa Tanzania Juma Jux baada ya wawili hao kuonekana wakiwa pamoja mara kadhaa.

Wawili hao hata hivyo walijitokeza kuweka wazi kuwa hakuna mahaba kati yao na kudai kwamba uhusiano wao ni wa kirafiki na kibiashara tu.