Mwanamitindo Paula Kajala augua homa kwa kumkosa mpenzi wake

Binti huyo wa Kajala Masanja alidai kuwa hali hiyo imetokana na kumkosa mpenzi wake.

Muhtasari

•Katika video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Paula alibainisha kwamba anaugua homa.

•Haya yanajiri siku moja tu baada ya aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Rayvanny kudokeza kwamba anajutia kutengana naye.

Image: INSTAGRAM// PAULA KAJALA

Mwanamitindo maarufu na mfanyibiashara wa nguo Paula Paula Kajala amedokeza kuwa ni mgonjwa.

Katika video ambayo inasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Paula alibainisha kwamba anaugua homa.

Binti huyo wa muigizaji mkongwe Kajala Masanja zaidi alidai kuwa hali hiyo imetokana na kumkosa mpenzi wake.

"Binti pole. Unaumwa nini kwani?" jamaa mmoja nyuma ya kamera anasikika akimwambia Paula kwenye video hiyo.

Paula alijibu, "Sijui, nammiss mpenzi wangu tu. Napata homa." 

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alirekodiwa akiwa ameketi kwenye sofa huku akitumia simu yake alionekana mgonjwa kwa kweli.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya aliyekuwa mpenzi wake, mwanamuziki Rayvanny kudokeza kwamba anajutia kutengana naye.

Siku ya Jumatano jioni, bosi huyo wa Next Level Music alichapisha picha ya kumbukumbu ya siku zake na Paula kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Rayvanny aliambatanisha picha hiyo yake na binti huyo wa muigizaji mkongwe Kajala Masanja wakiwa wameketi kwenye kiti na emoji ya uso uliofunikwa kwa kiganja cha mkono ambayo mara nyingi huashiria  kufadhaika au aibu.

Ingawa hakushiriki maelezo zaidi, emoji hiyo pengine ilikusudiwa kufupisha hisia zake za jumla kuhusu uhusiano wao uliovunjika.

Mwaka jana wakati akitumbuiza katika tamasha la Fiesta 2022 mjini Sumbawanga, Tanzania, Rayvanny alidokeza kusambaratika kwa mahusiano yake ya muda mrefu na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20.

Alidokeza hayo wakati akitumbuiza wimbo wake 'Naogopa' ambapo aliongeza mistari kadhaa iliyosikika kama ujumbe wa kukiri.

"Mapenzi yasikuchanganye nakwambia, usije ukapata bila kama Dulla. Mapenzi usije kufananisha,  kama  vile chakula. Nilinyosha moyo Karula, nikaachana na Paula..." aliimba.

Baadaye, msanii huyo wa zamani wa WCB alidaiwa kuzozana na Paula, madai ambayo alipuuzilia mwishoni mwa mwezi Oktoba.