Nadia Mukami na Arrow Bwoy wafichua waliovunja ubikira wao, uzoefu wao wa tendo la ndoa

Arrow Bwoy alionekana kushtuka sana na kulitilia shaka na jibu la mpenziwe lakini hatimaye alikubaliana naye.

Muhtasari

•Nadia amedai kuwa mchumba wake Ali Yusuf almaarufu Arrow Bwoy ndiye mwanaume wa kwanza kufanya naye mapenzi.

•“Nilipokuwa kidato cha pili, nilijaribu. Nilikuwa nachumbiana na mtukidato cha nne. Alikuwa bikra. Nilipambana. Sikufurahia," Arrow Bwoy alisema.

Image: INSTAGRAM// NADIA MUKAM

Malkia wa muziki wa Kenya Nadia Mukami amedai kuwa mchumba wake Ali Yusuf almaarufu Arrow Bwoy ndiye mwanaume wa kwanza kufanya naye mapenzi.

Wanandoa hao ambao wana mtoto mmoja mvulana walikuwa wakishiriki kipindi cha Maswali na Majibu kwenye mtandao wa YouTube wakati Nadia alipofanya ufichuzi huo.

"Nani alivunja ubikira wako?" Arrow Bwoy alimuuliza mpenzi wake.

Nadia Mukami alijibu haraka, na kwa utani "Wewe!" na mara akaangua kicheko kikubwa.

Mwanzoni, Arrow Bwoy alionekana kushtuka sana na kulitilia shaka jibu hilo lakini hatimaye akakubaliana na mzazi huyo mwenzake.

“Naipenda familia yangu, sina budi kuilinda familia yangu kwa moyo wangu wote. Ni mimi,” Arrow Bwoy alisema huku akikubaliana na jibu la Nadia.

Alipoulizwa kuhusu mara ya kwanza aliposhiriki mapenzi, Arrow Bwoy alisema, “Nilipokuwa katika kidato cha pili, nilijaribu. Nilikuwa nachumbiana na mtu ako katika kidato cha nne. Alikuwa bikra. Nilipambana, wueh, nilipamba. Sikufurahia. Ndio maana saa hii ukiniuliza, afadhali unipee gari iko na uzoefu kwa barabara kuliko unipee kitu ambacho kimetoka kwa duka. Saa hii uniletee bikra na wewe (Nadia), afadhali nikufe na wewe.”

Mwimbaji huyo wa kibao ‘Digi Digi’ pia aliulizwa kuhusu sehemu ya kushangaza zaidi ambayo aliwahi kufanyia tendo la ndoa.

Kwa gari, na kwa studio pia,” Arrow Bwoy alijibu.

Baba huyo wa mtoto mmoja pia alidai kwamba hawezi kukumbuka wazi jina la msichana wa kwanza ambaye alimpenda.

Wanamuziki hao wawili wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miaka minne iliyopita na hata wana mtoto mmoja mvulana pamoja, Haseeb Kai ambaye alizaliwa mapema mwaka jana.

Safari ya mapenzi ya wawili hao hata hivyo haijawa laini kwani katika siku za nyuma waliwahi kuachana nakurudiana. Pia kwa bahati mbaya walipoteza ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza kama bado hajazaliwa mwaka 2021.

Mwaka uliopita, Nadia alifichua kwamba aliamua kuzama kwenye mahusiano na Arrow Bwoy kwa vile alivyomtunza kama binti wao kifalme.

Mwimbaji huyo alikiri kuwa wamepitia mengi pamoja huku akisema anatazamia kuishi maisha yake yote pamoja na msanii huyo mwenzake.

"Nilisema Ndiyo kwa mpenzi wa maisha yangu Arrow Bwoy. Nilikupenda kwa sababu ya jinsi ulivyokuwa unanichukulia kama binti wa kifalme. Una Moyo wa Kustaajabisha zaidi. Moyo wako ni safi na siwezi kungoja kuishi maisha yangu yote na wewe. Tumepigana vita vingi sana pamoja. Watu wanaona msanii, mvulana mbaya. Ninaona mtu wa familia anayewajibika. Mwanangu ana bahati ya kuwa na wewe kama baba. Amebarikiwa sana. Nadhani wanaume wa familia yako wamelelewa vizuri kwa vile wanavyojibeba. Mungu ambariki mama yako.  Hata katika Maisha Yanayofuata, bado nataka kuwa nawe. Nakupenda Ali Etale. Malengo na ndoto zetu mwaka huu zinaanza Kudhihirika. Nataka kuwa tajiri na wewe ," Nadia alisema.

Mahusiano ya Arrow Bwoy na Nadia yalikuja kujikana hadharani mwaka wa 2021.