"Nakumiss!" Zari ashindwa kuficha upweke baada ya mpenziwe kuwa mbali naye

Mwezi uliopita Zari alimtambulisha mwanaume huyo kama mume wake.

Muhtasari

•Zari amekiri kwamba anamkosa mpenzi huyo wake ambaye ni machache tu yanayojulikana kumhusu.

• Mwezi uliopita Zari alimtambulisha mwanaume huyo, sio tu kama mpenzi wake, bali pia kama mume wake.

Zari Hassan
Image: Maktaba

Mwanasoshalaiti mashuhuri Zari Hassan  ameshindwa kuficha upweke baada ya kuwa mbali na kipenzi chake kwa muda.

Mama huyo wa watoto watano amekiri kwamba anamkosa mpenzi huyo wake ambaye ni machache tu yanayojulikana kumhusu.

Mnamo Alhamisi Zari alipakia picha ya mpenzi wa mpenzi wake ya kudokeza jinsi anavyotamani angekuwa karibu.

"Miss you!" Zari aliandika chini ya picha ya mwanaume huyo anayeripotiwa kuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Isitoshe mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alifuatisha ujumbe huo na emoji inayoashiria mtu mpweke.

Haya yanajiri takriban mwezi mmoja tu baada yake kuonekana na jamaa huyo aliyeuteka moyo wake katika ziara ya Kenya na Tanzania.

Akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kutua Tanzania, Zari alimtambulisha mwanaume huyo, sio tu kama mpenzi wake, bali pia kama mume wake.

“Huyu ni mume wangu, ni mume wangu, kesi kwisha!” Zari alisema

Mzaliwa huyo wa Uganda hata hivyo alikataa kufichua jina la mpenzi  wake wakati alipoombwa kufanya vile.

Licha ya kuwa aliandamana naye katika ziara yake, Zari aliweka wazi kwamba mume huyo wake anamheshimu na hajihusishi kamwe katika  kazi zake.za kazi.

“ Niko kwenye kazi na mume wangu wangu na haingilii vitu vyangu za kazi , ananiheshimu.” Alisema.

Hatua ya Zari kutambulisha mpenziwe mpya ilizua mdahalo mkubwa kwenye mitandao ya kijamiii huku baadhi ya wanamitandao wakimshtumu kwa kutoka kimapenzi na wanaume wadogo.

Kabla ya kujitosa kwenye mahusiano na mpenzi wake wa sasa, mwanasoshalaiti huyo alichumbiana na mfanyibiashara wa Uganda aliyetambulishwa kama GK Choppa. Hayo yalitokea mapema mwaka huu.