•Khalwal amemtupia lawama msanii huyo maarufu wa Kikuyu na kumshutumu kwa kushindwa kuwasimamia wake zake.
•Seneta huyo sasa ametoa wito kwa Wakenya kumpa Karen mapumziko na kuachana na yeye kabisa.
Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amemtaka staa wa Mugithi Samidoh kuomba msamaha kufuatia drama nyingi za hivi majuzi zinazomhusisha yeye, mzazi mwenzake Karen Nyamu na mke wake Edday Nderitu.
Hivi majuzi, Bi Karen na Edday nusura wapigane wakati wa tamasha lake la Mugiithi jijini Dubai mnamo Desemba 16, 2022.
Khalwale sasa amemtupia lawama msanii huyo maarufu wa Kikuyu na kumshutumu kwa kushindwa kuwasimamia wake zake. Huku akimtetea seneta mwenzake Karen Nyamu, Khalwale amebainisha kuwa mama huyo wa watoto watatu hana hatia na anapigania tu mwanamume anayempenda.
"Hapa kuna mwanamke mdogo ambaye anampenda mwanaume wake lakini kwa bahati mbaya jamaa huyo hajui jinsi ya kusimamia wake zake. Anapaswa kuomba msamaha kwa kutokuwa na uwezo katika masuala ya familia. Yeye ndiye wa kulaumiwa," Khalwale alisema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Seneta huyo sasa ametoa wito kwa Wakenya kumpa Karen mapumziko na kuachana na yeye kabisa.
"Ndoa ya wake wengi sio kwa wavulana!" Khalwale aionekana kumshambulia Samidoh.
Karen na Samidoh wamekuwa kwenye uhusiano uliojaa drama kwa muda na tayari wawili hao wana watoto wawili pamoja.
Jumapili, Karen alijitangaza mwisho wa uhusiano wake na mzazi mwenzake baada ya kuzozana na mkewe Edday Nderitu.
Baada ya kutafakari kwa makini kuhusu yaliyojiri, Karen alizamia kwenye mitandao ya kijamii na kujitangaza kuwa single, akisema amekatiza uhusiano na Samidoh.
"Wanawake wakubwa na wenye nguvu watathibitisha kwamba mara nyingi kiungo chetu dhaifu ni wanaume tunaojihusisha nao. Ninaacha mtindo huo. Nimefanya uamuzi wa kuhitimisha ushiriki wangu na baba wa watoto wangu na sasa ex Samidoh Muchoki."
“Ningeweza kumpigia simu Samidoh nikamaliza kimya kimya lakini nikaifanya drama, hili limekuwa jambo la kusumbua kwani mimi ni mbunge wa senati....Sijutii ila naahidi ndiyo mara ya mwisho kuhusika katika hali kama hiyo."
Sitamani ningefanya mambo tofauti. Hata hivyo nawaahidi kuwa ni mara ya mwisho kwa msichana wenu kuhusika katika hali kama hizo tena."
Aliongeza kuwa alibahatika kukabidhiwa heshima na jukumu la uongozi nchini.
"Kuwa mwakilishi wa wananchi bungeni ni fursa ninayoithamini na kuichukulia kwa uzito mkubwa."