"Ngotha.. ngotha ​​tena" Hisia mseto baada ya Brown Mauzo kumzawadi mpenziwe chupi za mwaka mzima

Wanamitandao wameendelea kutoa maoni mseto kuhusu chaguo la Brown Mauzo la zawadi ya kumpa mpenziwe, Kabianga Jr.

Muhtasari

•Mume huyo wa zamani wa mwanasosholaiti Vera Sidika alisema alitaka kum’surprise mpenzi wake kwa njia ya kipekee kwani anastahili.

•Kabianga alimshukuru mpenzi wake na kubainisha kuwa alikuwa amepata na chupi za kumhudumia kwa mwaka mzima.

na mpenziwe Kabianga
Brown Mauzo na mpenziwe Kabianga
Image: HISANI

Wanamitandao wameendelea kutoa maoni tofauti kuhusu chaguo la mwanamuziki Brown Mauzo la zawadi ya kumpa mpenzi wake Kabianga Jr.

Siku ya Jumanne, Mauzo alichapisha video ambayo ilimuonyesha akimpelekea mpenzi wake rundo la maua, chupa ya mvinyo na sanduku la zawadi.

Mume huyo wa zamani wa mwanasosholaiti Vera Sidika alisema alitaka kum’surprise mpenzi wake kwa njia ya kipekee kwani anastahili.

"Zawadi ndogo, ua la upendo, divai hapa kwetu, sio lazima igharimu pesa nyingi, inahitaji tu kum’surprise. Anastahili zaidi ya hii ..... Ukuu wake wa kifalme. Ilibidi nimfanye tu surprise,” Brown Mauzo aliandika chini ya video hiyo.

Baadaye Kabianga alionyesha maua aliyopokea kutoka kwa mpenzi wake na sanduku la zawadi kabla ya kulifungua.

“Kuna nini humu ndani?’” Kabianga alijiuliza kabla ya kulifungua sanduku lile.

Kisha mrembo huyo alionyesha video nyingine akifungua sanduku hilo ambalo lilikuwa limejaa chupi za aina na rangi tofauti.

“No way.. hizi zinakaa vizuri.. mbona anipe chupi nyingi,” alijiuliza huku akiendelea kuitoa ile chupi kwenye boksi.

Mtayarishaji huyo wa maudhui ya kidijitali hata hivyo alimshukuru mpenzi wake na kubainisha kuwa alikuwa amepata na chupi za kumhudumia kwa mwaka mzima.

"Chupi za mwaka mzima. Brownskin I am saving you sum @brownmauzo254,” alisema.

Video za zawadi hiyo ya kipekee zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watumiaji wa mtandao wameendelea kutoa maoni tofauti.

Baadhi ya wanamtandao wamepongeza zawadi hiyo ya kipekee, wengine wamekejeli kitendo hicho, huku wengine wakiwapongeza wapenzi hao.

Tazama maoni ya baadhi ya wanamtandao;

Kafuri_fx: Ngotha.. ngotha tena..

Djallybi: Wenzako tunapeana maGLC we unapeana chupi buda boss weekaapu

Msodoki.ke: Kwani alimpata na pantie imeraruka?

Thee_pluto: Pantie mia???

Tanashamuthoni: Very mindful, very cutesy

_ngairaa: Nkt kwani wanaanza biz ya masuruali??

St3.phanni_e: It’s low-key embarrasing.

_sandra_bellah: Jamani mauzo shikilia hapo she's sooo charming 😍😘🤗

felly_fits:You really put in the effort... very nice ❤️