Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee ametoa taarifa ya kutia wasiwasi kuhusu nyakati za kutisha ambazo amepitia katika miezi michache iliyopita.
Katika taarifa yake siku ya Jumapili jioni, mama huyo wa watoto watano alifichua kuwa amekuwa akihudhuria vikao vya ushauri maalum na mtaalamu wa kisaikolojia na kujaribu kupona faraghani kwa miezi miwili iliyopita katika juhudi za kurejesha afya yake ya akili.
Alifichua kwamba matatizo yote yalianza baada ya kupata ukweli fulani na maelezo fulani ya kutisha ambayo yalimfanya aingiwe na hofu na kumpelekea kuingia kwenye dimbwi la mawazo.
"Nimetoka eneo hatari sana na nimekuwa nikipona kwa faragha, niko kwenye mwezi wa pili wa therapy kufuatia kiwewe nilichopitia baada ya kujua ukweli na mambo mabaya ambayo yaliniacha nikitetemeka, Zilipita siku bila chakula. na hakuna kulala, nilihoji na kujijibu mwenyewe, imekuwa nzito sana. Siku zingine, usiku ungekuwa siku na kuniacha mimi nikitazama nje ya dirisha nikikadiria yasiyokuwepo, ningejipata nikitetemeka kwa sababu ambazo siwezi kuelezea, na kumbuka bado nilikuwa na kazi ya kufanya, familia na ufalme wa kulinda. Bado nililazimika kuweka uso mkali na kuwaburudisha mashabiki wangu,” Akothee alisema kupitia mtandao wa Facebook.
Aliwashukuru wote waliosimama naye wakati wa nyakati ngumu alizopitia na kumsaidia kutembea katika safari ya uponyaji ikiwa ni pamoja na marafiki wake wa karibu, familia na meneja wake Nelly Oaks ambaye amemtaja kama rafikiye mkubwa.
"Nelly Oaks amekuwa akipiga simu haraka, akinipigia bila kukoma na alikuwa akiogopa simu yangu ilipokatika, watoto wangu kisawa sawa hasa wasichana tulihakikisha tunaweka timer ili kuangalia kama niko sawa. Rue alinifuata Ulaya kwa hofu. ya kunipoteza, mtoto alinikalisha hadi nikasimama kwa miguu yangu,” alisema mwimbaji huyo.
Aliongeza, "Nilianza kwa kufuatilia mienendo yangu, niligundua kuwa nilikuwa nikilemewa na hisia mara kwa mara bila sababu, hata mahojiano rahisi tu. Nilikuwa nimekosa utulivu, na sikuweza kuweka kidole juu yake. Sikuwahi kujua kuhusu Unyanyasaji wa Kihisia, hadi nilipoanza matibabu. Nilikuwa katika hali mbaya ya akili iliyonifanya nilipe ksh 50,000 kwa saa kwa kipindi cha saa moja na mtaalamu wa kwanza. Nilikuwa nikitetemeka na kupoteza nguvu, hamu ya kula, usingizi, hofu na hata kupoteza motisha katika kufanya mambo niliyopenda kufanya.”
Kufuatia hilo, amewaomba watu kuendelea kumuunga mkono na kumuombea yeye na familia yake wakati wakiendelea kurekebisha mambo faraghani.