"Sikuhitaji kueleza chochote" Mimi Mars asema kuhusiana na Marioo kuumia baada yake kuogelea na Diamond

Muhtasari

•Malkia huyo  ambaye ni dada wa Vanessa Mdee ameshikilia msimamo kuwa uhusiano wake na Marioo ni wa kirafiki tu.

•Mars pia alifichua kuwa hakuwahi kujua kuwa tukio la yeye kuonekana kwenye bwawa la kuogelea na Diamond lilimuumiza Marioo

Marioo na mpenzi wake Mimi Mars
Marioo na mpenzi wake Mimi Mars
Image: INSTAGRAM// MARIOO

Mwanamuziki na mtangazaji Mimi Mars amesisitiza kuwa hakuna uhusiano wa kimapenzi kati yake na Marioo.

Malkia huyo  ambaye ni dada wa Vanessa Mdee ameshikilia msimamo kuwa uhusiano wake na Marioo ni wa kirafiki tu.

"Mimi na Marioo hatupo kwenye mahusiano. Tuna mahusiano ya kirafiki ambayo ni mazuri. Nahisi hicho dicho kinasababisha watu kusema tupo kwenye mahusiano," Mars alisema katika mahojiano na Wasafi Media.

Mars hata hivyo hakutupilia mbali uwezekano wa wao kujitosa kwenye mahusiano katika siku za usoni.

"Wakati mwingine urafiki huko mbeleni mambo yakikorea yanaweza kuwa mazuri lakini ikitokea mtajua. Sisi wenyewe ndio tutasema lakini kwa sasa hamna kitu," Mars alisema.

Hata hivyo aliweka wazi kuwa tayari yupo kwenye mahusiano mengine na mwanaume ambaye sio maarufu. Alifichua kuwa mpenzi wake ni raia wa Tanzania.

Alieleza kuwa alikuja kufahamu kuhusu hayo hivi majuzi wakati Marioo alifunguka kupitia Instastori zake.

"Sidhani kama nilihitaji kumweleza chochote. Sikujua chochote muda huo eti angeumia. Mimi mwenyewe nilikuja kujua juzi alipoweka kwenye Instastori zake. Hakuwahi kuniambia," Alisema.

Hata hivyo aliweka wazi kuwa hakukerwa na hatua ya Marioo kufunguka kuhusu hisia zake kufuatia tukio hilo.