Sio kiki! Vera Sidika hatimaye avunja kimya kuhusu kutengana na Brown Mauzo

Mama huyo wa binti mmoja alibainisha wazi kwamba hatumii utengano kutafuta kiki.

Muhtasari

•"Sio kila utengano husababishwa na usaliti wa kimapenzi. Kuna mambo mengi yanayochangia," Vera alisema.

•Alisema huwa hatumii utengano kama njia ya kutafuta kiki kwani inaweza kuathiri mahusiano kwa njia moja au nyingine.

Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: Vera Sidika Instagram

Mwanasosholaiti wa Kenya Vera Sidika hatimaye amevunja kimya kuhusu madai ya kutengana na mzazi mwenzake Brown Mauzo.

Katika taarifa yake siku ya Jumatano, mama huyo wa binti mmoja alibainisha wazi  kwamba hatumii utengano kutafuta kiki.

"Sijawahi kufanya kutumia utengano kutafuta kiki kwa zaidi ya miaka 5. Nimekuwa na mawazo ya kipekee ikiwa nataka kutafuta kiki na nyote mnajua, sio hii. Tafadhali acheni kulazimisha," Vera alisema kupitia Instagram.

Alibainisha kwamba utengano sio mojawapo ya mbinu ambazo yupo tayari kutumia kutafuta kiki wakati wowote anapohitaji.

"Lolote linakalotokea, hutokea katika maisha halisi. Na ikiwa haukujua, sio kila utengano husababishwa na usaliti wa kimapenzi. Kuna mambo mengi yanayochangia," alisema.

Aliongeza, "Maisha hutokea. Watu hutengana a na kuendelea. Baadhi hutengana na kutatua mambo. Ndivyo maisha yalivyo. Kamwe sio safari laini."

Mwanasosholaiti huyo alidokeza kwamba amejifunza mengi kutokana na mahusiano yake ya awali ambayo yalimfanya kushughulikia mambo kwa njia tofauti wakati alipokatiza mahusiano na wapenzi wake wa hivi majuzi.

"Lakini jambo moja kuhusu mimi, tangu ukuaji kutoka kwa mahusiano ya zamani, sijawahi kufanya hii kazi. Ndio maana hakuna hata aliyejua nilipomalizana na ex wa Senegal, Mtanzania hadi miezi kadhaa baadaye," alisema.

Alisema hawezi kutumia utengano kama njia ya kutafuta kiki kwani inaweza kuathiri mahusiano kwa njia moja au nyingine.

"Ni aidha tumeachana au la. Au tuliachana na baadaye kusuluhisha masuala. Sio kuachana kwa ajili ya kiki. Ni ya kitoto na ya kuchosha," alisema.

Siku za hivi majuzi, kumekuwa na uvumi kuwa ndoa ya Vera na Mauzo ya zaidi ya miaka imefika kikomo. Hii ni kutokana na matendo ya wawili hao kwenye mitandao ya kijamii na kwa kuwa hawajaonekana pamoja kwa muda.