Trio Mio afunguka kuhusu kuchumbiana na mwanamke mzee

"Inategemea uhusiano. Lakini sitawahi kuchumbiana na mwanamke mzee," alisema.

Muhtasari

•Katika mahojiano na Mungai Eve, Trio Mio alibainisha kuwa anawaheshimu wanawake walio juu yake kiumri.

•Rapa huyo mdogo alimmwagia sifa mpenzi wake.

Trio Mio
Image: Instagram

Mwimbaji mdogo wa muziki wa kisasa Trio Mio anasema babake alimshauri asiwahi kuchumbiana na mwanamke mzee.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Trio Mio alibainisha kuwa anawaheshimu wanawake walio juu yake kiumri.

"Inategemea uhusiano. Lakini sitawahi kuchumbiana na mwanamke mzee. Ni ukweli," alisema.

"Tukiwa umri sawa zogo inaweza zua, mnaeza katsiana vibaya sana na mimi staki, so nitachumbiana na mtu ambaye ni mdogo kuliko mimi."

Mwaka wa 2021, mama yake, Irma Sakwa, alisema kuwa alikutana na mpenzi wa Trio na kuidhinisha.

"Nilifurahi angalau ameleta msichana na nimekutana naye. Ni vizuri. Ni bora kuliko kuweka uhusiano kuwa siri."

Rapa huyo mdogo alimmwagia sifa mpenzi wake.

"Yeye ni mrembo, ananifurahisha, ni msikivu," alisema.

"Nataka kufikia malengo yangu kwani yeye anafanikisha yake tukiwa bado pamoja."