(+Video) Mapacha! Diamond afurahia muda na mtoto wake na Tanasha Donna

Muhtasari

•Wawili hao ambao wanafanana kama shilingi kwa ya pili walionekana wakicheza na vinyago huku wakishiriki mazungumzo mazuri kwa Kiingereza.

•Video moja ilimuonyesha Diamond akiwa amemshika mwanawe huku wakijirekodi kutumia kamera ya selfie.

Diamond na Naseeb Juniour
Diamond na Naseeb Juniour
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa Bongo Diamond Platnumz yupo nchini Kenya kwa ziara ya siku kadhaa.

Bosi huyo wa WCB aliwasili humu nchini siku ya Jumatano ila hakutoa maelezo mengi kuhusu ziara yake.

Diamond alikuwa ameandana na mmoja wa mameneja wake, Don Fumbwe pamoja na kikosi cha walinzi wenye miraba minne.

Chapisho lake la hivi punde kwenye Instagram limeashiria kuwa sababu moja ya kuzuru Kenya ilikuwa kumuona mtoto wake na  aliyekuwa mpenzi wake, Tanasha Donna.

Msanii huyo alipakia video inayoonyesha akifurahia muda na mwanawe Naseeb Junior huku wakichapa stori kama watu waliozoeana kwa muda mrefu.

Wawili hao ambao wanafanana kama shilingi kwa ya pili walionekana wakicheza na vinyago huku wakishiriki mazungumzo mazuri kwa Kiingereza.

Video nyingine ilimuonyesha Diamond akiwa amemshika mwanawe huku wakijirekodi kutumia kamera ya selfie.

"Mvulana mzuri aje.. Tabasamu N.J," Simba alisikika akimwambia Naseeb Juniour kwenye video hiyo.

Aliiambatanisha na ujumbe mfupi, "Mapacha ❤❤ Naseeb Juniour."

Hatua hii ya Diamond inapuuzilia mbali madai kuwa huwa hawashughuliki watoto wake wengine kama anavyowashughulikia wake na Zari Hassan.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi nyingi kuwa mwanamuziki huyo anawapendelea zaidi Tiffah Dangote na Prince Nillan.

Baba huyo wa watoto wanne wanaojulikana amekuwa akiwasherehekea wawili hao zaidi ya jinsi anavyowasherehekea Naseeb Junior na Dylan ambaye alipata na Hamisa Mobetto.

Diamond pia amekuwa akiwatembelea watoto wake na Zari mara kwa mara nchini Afrika Kusini ambako wanaishi kwa sasa.