Zari aonyeshwa mahaba mazito na mpenzi wake Shakib licha ya kudaiwa kumuacha

"Kheri ya siku ya Valentino malkia wangu, wewe ni baraka kwangu," Shakib alisema.

Muhtasari

•Shakib ametumia siku ya Valentino kumkumbusha mama huyo wa watoto watano kuhusu umaalum wake kwake.

•Zari aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Jumanne, Februari 14, ikiwa ni Siku ya Wapendanao, wapenzi kote ulimwenguni wameendelea kusherehekeana na kuthaminiana kwa njia tofauti.

Baadhi wamewazawadia wapenzi wao maua na vitu vingine vya thamani, wengine wanapanga kuwapeleka date wapenzi wao, wengine wametuma meseji tamu za mahaba  kwa wapenzi wao miongoni mwa vitendo vingine maalum ambavyo watu wamefanya kueleza mahaba yao mazito kwa wapenzi wao.

Mpenzi wa mwanasoshalaiti maarufu wa Uganda  Zari Hassan, Shakib Lutaaya, hajaachwa nyuma. Shakib ametumia siku ya Valentino kumkumbusha mama huyo wa watoto watano kuhusu umaalum wake kwake.

"Kheri ya siku ya Valentino malkia wangu, wewe ni baraka kwangu," Shakib aliandika chini ya picha yake na mwanasoshalaiti huyo.

Zari hata hivyo bado hajatuma ujumbe wowote wa Valentino kwa mpenziwe huyo mwenye umri wa miaka 31 kufikia wakati wa kuchapisha ripoti hii.

Ujumbe wa Shakib umeendelea kutupilia mbali wasiwasi uliokuwepo takriban mwezi uliopita kuwa mahusiano yao yamegonga ukuta.

Wapenzi hao walidaiwa kuenda njia tofauti mwezi uliopita baada ya kutoonekana pamoja kwa kipindi kirefu kirefu kama ilivyokuwa hapo awali. Tetesi hizo zilienea zaidi mwishoni mwa mwezi Januari wakati raia hao wawili wa Uganda walipochapisha jumbe za kimafumbo kwenye mitandao ya kijamii.

Zari aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake na Shakib baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

Baadhi ya watu hawaelewi jinsi uwongo unaweza kuwa sumu. Uongo huambukiza na kulaani mahusiano yenye furaha hadi unahisi kuumwa na tumbo kwa kuwaamini tena,

Haijalishi ni kiasi gani unampenda mtu, wakati mwingine huwezi kujizuia kujisikia kama aliiba Faraja yako. Huna raha tena kwa sababu unakisia kila kitu. Sasa, kuwaamini sio kazi rahisi. Sasa inahitaji bidii na wakati mwingine hiyo inachosha ilisomeka nukuu hiyo ya Horacio Jones ambayo alichapisha kwenye Snapchat.

Wiki chache zilizopita hata hivyo, mwanasoshalaiti huyo hata hivyo alizika tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake baada ya kuchapisha video zake na Shakib wakifurahia nyakati za kimapenzi pamoja

Kwenye akaunti yake wa Snapchat, mzazi mwenza huyo wa staa wa Bongo Diamond Platnumz alichapisha video inayomuonyesha akimuaga Shakib ambaye alikuwa akielekea mahali pengine ambapo hawakuficha.

"Tuonane hivi karibuni. Nakupenda,"  alisikika akisema kwenye video hiyo.

Shakib vilevile alimhakikishia mama huyo wa watoto watano kuhusu mapenzi yake makubwa kwake na kumuaga kwaheri.

"Kwaheri mpenzi wangu. Nakupenda," alisema.

Wapenzi hao wawili pia walionekana wakikumbatiana na kubusu midomoni walipokuwa katika uwanja wa ndege.