Zifahamu sifa 5 kuu zinazomvutia Zari Hassan kwa mwanaume

Wapenzi wengi wa zamani wa mwanasoshalaiti huyo wanaojulikana wamebainika kuwa na umri mdogo kuliko yeye

Muhtasari

•Wapenzi wake wengi wa zamani ambao wanajulikana wameonekana kuwa na sifa sawa au zinazokaribiana sana.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Siku za hivi majuzi mwanasoshalaiti wa Uganda Zari Hassan amekuwa akionyesha wazi kuwa yupo kwenye mahusiano.

Bila wasiwasi, mama huyo wa watoto watano amekuwa akimuonyesha mpenziwe wa sasa ambaye bado hajatambuliwa.

Ingawa amekuwa akionyesha picha zake na mpenziwe kwenye mitandao ya kijamii, Zari hata hivyo hajakuwa akitoa maelezo mengi kumhusu.

Tangu alipomfichua mpenzi huyo wake, Zari amekuwa akishambuliwa sana na wanamitandao suala kuu likiwa tofauti ya umri kati yake na mpenzi wake.

Mpenzi mpya wa mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 41  anaaminika kuwa mdogo zaidi kuliko yeye.

Hata hivyo tayari amewajibu wakosoaji wake kwa kuwaeleza  kuwa uamuzi wa nani wa kuchumbiana uko kwake pekee.

"Ukiniambia nichumbie nani na nisichumbie nani, nawajua wa aina hizo. Lakini hapa ndipo ninapoamua kubaki. Ni nini kinachokufanya ufikiri kwamba watu wengine hawana hadhi?... "Niko hapa kwa sababu nataka kuwa hapa, sio kwa sababu mnataka kunichagulia mahali pa kuwa," Zari alisema hivi majuzi.

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Mpenzi wa Zari wa sasa hata hivyo sio wa kwanza mdogo ambaye amewahi kujitosa kwenye mahusiano naye.

Wapenzi wake wengi wa zamani ambao wanajulikana wameonekana kuwa na sifa sawa au zinazokaribiana sana.

Sifa hizi ni pamoja na:-

1. Ni wadogo kuliko yeye

Wapenzi wengi wa zamani wa mwanasoshalaiti huyo  wanaojulikana wamebainika kuwa na umri mdogo kuliko yeye.

Hawa ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye ni mdogo wake kwa takriban miaka kumi, King Bae, GK Choppa, Dark Stallion na mpenzi wake wa sasa.

Aliyekuwa mume wake, marehemu Ivan Semwanga hata hivyo alikuwa amempiku umri kwa miaka mitatu.

2. Ni wenye misuli

Ni wazi kuwa akriban wanaume wote ambao wanajulika kuwahi kuwa kwenye mahusiano na mwanasoshalaiti huyo wamejenga misuli kweli.

Zari ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume wanaopenda kufanya mazoezi na wenye misuli  tinginya.

Mara nyingi mwanasoshalaiti huyo pia ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume warefu.

3. Wenye ngozi ya chokoleti

Zari na GK Choppa
Image: Instagram

Wapenzi wengi wa zamani wa Zari wameonekana kuwa na ngozi yenye rangi nyeusi na mguso kidogo wa kahawia.

Hawa ni pamoja na marehemu Ivan, Diamond, Dark Stallion, GK Choppa na mpenzi wake wa sasa

4. Wachapa kazi

Zari Hassan ameonekana kuvutiwa zaidi na wanaume wenye bidii kubwa  na malengo makubwa ya kimaisha.

Ingawa sio maelezo ya kazi ya wapenzi wake wote ambayo yapo wazi, yale yanayojulikana yamedokeza kuwa mama huyo wa watoto watano anapendelea wanaume wanaojituma zaidi maishani.

Marehemu Ivan Semwanga alikuwa mfanyibiashara mkubwa, sawa na GK Choppa na Diamond Platnumz ambaye ni msanii tajika pia.

Zari na aliyekuwa mume wake marehemu Ivan Semwanga
Image: HISANI

5. Wapenda anasa

Wapenzi wengi wa Zari wamebainika kuwa watu wasiojifungia na wanaopenda burudani za aina tofauti tofauti.

Zari ambaye pia ni wazi anapenda raha ameonekana mara nyingi akijivinjari na wanaume anaochumbiana nao katika maeneo ya burudani.

Akizungumza hivi majuzi, Zari alitangaza kuwa maisha yake hayafungwi na sheria zilizowekwa na jamii.

Mwanasoshalaiti huyo alibainisha kuwa yuko na haki kamili ya kumchagua yule ambaye angependa kuchumbiana naye.

Zari ambaye alionekana kughadhabishwa sana alisema yuko na haki kamili ya kumchagua yule ambaye angependa kuchumbiana naye.