Zuchu amthamini mpenziwe kwa ujumbe mtamu siku ya Valentine's

Muhtasari

•Staa huyo kutoka Zanzibar alimtaja mpenzi wake kama mtu muhimu sana katika maisha yake na kumtakia kheri njema za siku ya wapendanao.

• Alikuwa ameandamana na mdosi wake katika WCB Diamond Platnumz alipoelekeza ujumbe huo mtamu  kwa mpenzi wake.

ZUCHU
ZUCHU
Image: instagram/zuchu

Usiku wa Jumatatu malkia wa Bongoflava Zuhura Othman almaarufu kama Zuchu aliandalia wapendanao tamasha kubwa katika jukwaa la Milimani City, jijini Dar es Salaam.

Kwa vile ilikuwa siku maalum kwa wapendanao, Zuchu hakusazwa nyuma katika kudhihirisha huba kwa mpenzi wake ambaye kamwe hajawahi kutambulisha. 

Akizungumza na Wasafi Media, staa huyo kutoka Zanzibar alimtaja mpenzi wake kama mtu muhimu sana katika maisha yake na kumtakia kheri njema za siku ya wapendanao.

"Happy Valentines mpenzi na shukran kwa kila kitu. Wewe ni wa ajabu na wewe ni wa maana kubwa kwangu" Zuchu alisema.

Zuchu alikuwa ameandamana na mdosi wake katika WCB Diamond Platnumz alipoelekeza ujumbe huo mtamu  kwa mpenzi wake.

Hii huenda ilikuwa ishara wazi kwamba wababe hao wawili wa muziki hawachumbiani, kinyume na uvumi ambao umekienea katika kipindi cha wiki chache ambacho  kimepita.

"Mpenzi wangu ananitazama kutoka mahali alipo" Alisema Zuchu.

Katika kipindi cha wiki kadhaa ambacho kimepita uvumi umekuwa ukitanda kwamba Diamond tayari amemchumbia Zuchu na wanapanga kufunga pingu za maisha.

Kila mmoja wao hata hivyo amejitokeza kueleza kwamba uhusiano wao ni wa kikazi tu na sio wa mapenzi.