Zuchu amtukana Diamond vibaya baada ya kumbusu kimahaba kipusa wa Ghana, Fantana

Diamond alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

Muhtasari

•Pamoja na picha zake, Zuchu aliambatanisha video fupi ya mwanamuziki akiimba maneno mazito ya matusi.

•Diamond aliweka wazi kuwa busu la Fantana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya maisha yake.

katika ziara yao ya Ufaransa.
Diamond Platnumza na anayedaiwa kuwa mpenziwe, Zuchu katika ziara yao ya Ufaransa.
Image: INSTAGRAM// ZUCHU

Malkia wa muziki wa Bongofleva Zuhura Othman almaarufu Zuchu anaonekana kujawa na ghadhabu baada ya anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa zamani na ambaye ni bosi wake, Diamond Platnumz kuonekana akimbusu mwanamke mwingine katika sehemu ya pili ya filamu halisia ya Young, Famous na Africa.

Jumamosi, siku moja tu baada filamu  hiyo kupeperushwa kwenye Netflix, mwimbaji huyo wa kibao  'Sukari' alichapisha picha zake kadhaa kwenye mtandao wa Instagram. Pamoja na picha hizo, aliambatanisha video fupi ya mwanamuziki akiimba maneno ya matusi ambayo huenda tusiweze kuchapisha hapa.

Wengi wa wafuasi wake walionekana kutilia maanani sana video hiyo na hata kuihusisha na maendeleo ya hivi punde. Kwa kutaka kujua iwapo video hiyo na matukio ya filamu hiyo yanahusiana, binamu yake Diamond, Romy Jons alichukua hatua ya kumuuliza binti huyo wa Khadija Kopa ikiwa tayari ameshaitazama.

"Umeangalia msimu mpya wa filamu ya Dai? " Romy Jons alimuuliza Zuchu.

Msanii huyo wa WCB aliyeonekana kukerwa na swali hilo alijibu, "Nimeangalia mwaya mwambie nimesema F++k you."

Zuchu na bosi huyo wake walidaiwa kuwa wapenzi kwa muda mrefu hadi walipothibitisha kuachana Februari mwaka huu.

Huku akitangaza kutengana kwao mapema mwaka huu, Diamond aliweka wazi kwamba yeye na Zuchu sio wapenzi tena. Alibainisha yeye na malkia huyo wamebaki kuwa kaka na dada licha ya awali kuonyesha mahaba  makubwa kati yao.

"Kwa pamoja na Zuhura tunaomba tuwataarifu ya kwamba, kwa sasa sisi ni dada na kaka na si wapenzi kama ilivyokuwa ikidhaniwa ama wengine kujua.. Mnaruhusiwa wachumba na wake ama waume kama tutawaridhia," alisema.

Diamond aliongeza, "Lakini muwe na vibarua vinavyoeleweka  sio mje kutuchuna, maana atuhongi hovyo."

Katika moja ya matukio kwenye filamu ya Young Famous and African, Diamond alionekana akibusiana kimahaba na mwanamuziki wa Ghana Francine Koffie almaarufu Fantana

“Nilijiona mimi ndiye bora kwa kubusu, hadi nilipombusu Fantana,” Diamond alisema kuhusu tukio hilo la kubusiana.

Alibainisha kuwa busu la Fantana lilikuwa zaidi ya busu.

"Hakuwa ananibusu, alikuwa akinila!" alisema.

Diamond aliweka wazi kuwa busu la malkia huyo wa Ghana lilikuwa bora zaidi kuwahi kupokea katika miaka yote 32 ya kuwepo kwake.