Diamond Platnumz akiri upendo mkubwa kwa mrithi wake, Naseeb Junior

Wawili hao walivalia kanzu nyeusi zinazofanana na walionekana kuwa na muungano mzuri.

Muhtasari

•Diamond alionekana hadharani na mtoto huyo wake na Tanasha Donna kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.

•Mwezi Desemba, Mama Dangote  aliweka wazi kuwa Naseeb ndiye mrithi rasmi wa Diamond katika biashara ya Wasafi.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Wikendi iliyopita, staa wa Bongo Diamond Platnumz alishiriki muda mzuri na mwanawe mdogo, Naseeb Junior.

Diamond alionekana hadharani na mtoto huyo wake na Tanasha Donna kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu siku ya Jumamosi walipohudhuria hafla ya kumtambulisha mtoto wa mwanaspoti Haji Manara.

Siku ya Jumatatu, bosi huyo wa WCB alichapisha picha zake na mwanawe ndani ya gari lake la kifahari aina ya Rolls Royce. Wawili hao walivalia kanzu nyeusi zinazofanana na walionekana kuwa na muungano mzuri.

"@naseeb.junior❤️🌹," aliandika chini ya picha hizo ambazo alipakia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Picha zingine zilimuonyesha akiwa amemshika mvulana huyo wa miaka mitatu.

Diamond mara nyingi ameonyesha upendo mkubwa kwa mvulana huyo mdogo aliyempata na mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna. Wawili hao walichumbiana kwa muda mfupi kabla ya kutengana mwaka wa 2019.

Naseeb Junior anatabiriwa kuwa mrithi anayependekezwa wa mwimbaji huyo tajiri maarufu kutoka Kigoma, Tanzania. Mama yake, Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote hata alidokeza kuhusu hilo mwaka jana.

Mwezi Desemba, Mama Dangote  aliweka wazi kuwa Naseeb ndiye mrithi rasmi wa Diamond katika biashara ya Wasafi.

Mama Dangote ya Diamond akiwa na mwanawe huyo na kusema kuwa amemkabidhi kijiti cha kuwa mrithi wake.

Mr. Tom kaka mdogo leo namkabidhi kijiti cha wasafi 👬Mimi mwenyewe,” Mama Dangote alitangaza bayana.

Mwezi Julai mwaka jana,  Tanasha Donna aliweka wazi kuwa matamanio yake ni mwanawe kuwa mwanaspoti.

Katika mahojiano na Mpasho, Tanasha alisema hangependa Naseeb awe mwananamuziki kama yeye na mzazi mwenzake Diamond Platnumz.

Alieleza kuwa katika siku za usoni angependa sana mtoto huyo wake wa pekee ajihusishe na michezo kama vile soka badala ya muziki.

"Nahisi kama kuna uwezekano. Mama yake ni mwimbaji na baba yake ni mwimbaji. Kuna uwezekano mkubwa wa yeye kufuata njia hiyo, Mungu pekee ndiye ajuaye. Ingekuwa kwa matakwa yangu, ningemtaka awe mwanasoka," Tanasha alisema.

Mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alibainisha kuwa kimsingi, wanamichezo huwa na nidhamu sana tofauti na wanamuziki.

"Najua watu wanaojihusisha na michezo wana nidhamu sana. Wanaamka mapema, wanafanya mazoezi, wanakimbia, hawanywi pombe kwa sababu kuna vipimo vinavyofanywa kila wakati. Ingekuwa juu yangu, ningetaka hivyo kwa sababu tasnia hii ya muziki inakuja na mengi. Kuna siasa nyingi nyuma yake," Alisema.

Aliongeza "Kuna mengi ambayo huendelea katika tasnia ya muziki. Ukiwa una ushawishi na uko na pesa nyingi, unaweza kuendesha mambo mengi. Ndivyo hukuwa kwenye tasnia nyingi. Hata hivyo naamini kila tasnia huja na mazuri yake na mabaya yake. Hata michezo huwa na upande wake mbaya," 

Tanasha hata hivyo alidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mwanawe huyo kufuata nyayo zake na Diamond.

Aliweka wazi kuwa ikitokea Naseeb awe mwanamuziki basi hatasita kuunga mkono taaluma yake na kumsaidia kuikuza.

"Lakini ikitokea afanye muziki nitamuunga mkono kikamilifu na nitakuwa na uzoefu wa kumwelekeza katika njia sahihi. Acha tuone, muda utasema," Alisema.