logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia mseto baada ya msanii Embarambamba kuachia wimbo mpya"nataka kupupu" (+video)

Embarambamba alichapisha sehemu ya wimbo wake kwa jina ‘Nataka Kupupu’ ambapo anaimba kuhusu kuungama dhambi zake na kutubu.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani22 July 2024 - 09:12

Muhtasari


  • •Embarambamba alichapisha sehemu ya wimbo wake kwa jina ‘Nataka Kupupu’ ambapo anaimba kuhusu kuungama dhambi zake na kutubu.
  • •Wakenya wametoa maoni mseto huku wengi wakimkosoa, wengine wakimuunga mkono huku wengine wakicheka kuhusu maneno ya wimbo huo.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamezua mjadala mwingine kuhusu mwimbaji wa nyimbo za Injili mwenye utata, Christopher Mosioma almaarufu Embarambamba,  kufuatia wimbo wake wa hivi punde.

Mwimbaji huyo kutoka eneo la Kisii hivi majuzi alichapisha sehemu ya wimbo wake kwa jina ‘Nataka Kupupu’ ambapo anaimba kuhusu kuungama dhambi zake na kutubu.

Katika video ya wimbo huo, anaonekana akiwa amepiga magoti mbele ya madhabahu katika kanisa moja huku akiwa ameshikilia Biblia na bendera ya Kenya.

“Na kwa mbele yako Baba, niko na dhambi (*3), na mimi nitakataka kwa uso wako (*2). Nataka nipupu (*2), nataka kupupu (dhambi) (*4), nimekaziwa na dhambi, eeh Mungu nisaidie (*2),” Embarambamba alisikika akiimba kwenye kipande cha video ya wimbo wake kabla ya kutangaza kuwa ni kibao kipya cha injili ambacho atatoa hivi karibuni.

‘Kupupu’ ni neno la sheng linalotumiwa sanasana na Wakenya hasa kumaanisha kwenda haja kubwa.

Wakenya kwenye mitandao ya kijamii, hata kama hawajashangazwa sana na maneno ya wimbo wa Embarambamba, hata hivyo wametoa maoni mseto huku wengi wakimkosoa, wengine wakimuunga mkono huku wengine wakicheka kuhusu maneno ya wimbo huo.

Tazama maoni kutoka kwa baadhi ya Wakenya kwenye mtandao wa Twitter;

@Rhymaholic: Huyu sasa huimba nini. Kuna vitu mingi zilimpita akiwa babyclass.

@Inganga_Fre: This man should leave the country now.

@kelvintoo14GMA1: I think this guy needs to be stopped.

@sagarakelvin2: Mzee ameshiba saai ni kutapika tu.

Bill_valar: He needs to be restored.

MalcomX56971: Anataka kupupuu kanisani jameni..

Mapema mwaka huu, Embarambamba, alijitokeza kuomba msamaha baada ya Bodi ya Filamu na Uainishaji nchini (KFCB) kumuagiza kuzifuta video zote zenye maudhui chafu kwenye chaneli yake ya mtandao wa YouTube kwa kile ambacho shirika hilo lilisema ni maudhui chafu yanayoharibu maadili ya jamii.

Katika video fupi iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Embarambamba aliisihi KFCB kutomchukulia hatua, akisema watoto wake watateseka ikiwa maudhui yake yataondolewa kwenye majukwaa ya mtandaoni.

Alisema anategemea tu maudhui yake kwa mapato, ambayo yeye hutumia kulisha familia yake, na hatua ya hivi punde ya KFCB itawatia matesoni.

"Tafadhali naomba msamaha, kwa sababu ile barua mmeniwekea kwa mkono wangu ni nzito. Najua bianadamu aliyezaliwa na mwanamke hawezi kosa kufanya makosa, na huomba msamaha," Embarambamba aliomba.

Pia alitangulia kuomba msamaha kutoka kwa Wakenya, akisema yeyote aliyekerwa na nyimbo na maudhui yake, anapaswa kupata moyoni mwao kumsamehe.

"Mimi nilijua nafanya nyimbo hizi za Mungu watoto wangu wasome, wakule vizuri na mimi nikae vizuri kwa maisha yangu. Lakini Wakenya, sina uwezo," aliongeza.

Embarambamba alikiri zaidi kwamba kile ambacho amekuwa akifanya mtandaoni si sahihi, akisema anatarajia kubadilisha maudhui yake ili kuakisi matarajio ya jamii.

"Mngeniskiza. Kuliko nidelete nyimbo zangu kutoka Youtube, mnibakishie kidogo ili nisomeshe watoto wangu na wapate kitu cha ukubwa. 6.4 million views yote jamani?" alizidi kuomba.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved