'Tafadhali nisameheni,'Omosh aomba wakenya msamaha

Muhtasari
  • Muigizaji Omosh awaomba wakenya msamaha
  • Wakenya wengi waligadhabishwa na Omosh baada ya video yake akiwa mlevi chakari kuenea mitandaoni
Joseph Kinuthia
Image: Ivy Muthoni

Muigizaji Joseph Kinuthia maarufu Omosh akiwa kwenye mahojiano siku ya Jumanne aliomba wakenya msamaha baada ya video yake akiomba msaada tena kuibuka.

Wakenya wengi waligadhabishwa na Omosh baada ya video yake akiwa mlevi chakari kuenea mitandaoni, huku wengi wakimkejeli na kusema wanapaswa kuenda 'Rehab'.

Huku akizungumza na mpasho Omosh alidai kwamba video hiyo ni ya kitambo na kwamba watu wanaitumia kwa manufaa yao wenyewe.

Pia akiwa kwenye mahojiano na Hiram Maina, Omosh aliwaomba Wakenya msamaha kufuatia video ambayo inaenea mitandaoni ambayo inamuonyesha akiomba pesa tena.

"Kama msanii, unaweza kutoa taarifa tu na watu huchukulia kwa uzito. "ilikuwa jambo kidogo lakini Wakenya walinisaidia sana, walinisadida wakati wangu mgumu

Tafadhali naomba msamaha  niliwaumiza. Na asanteni kwa kunisamehe. Sikujua wala kufikiria Wakenya wangekasirika.

Ninajisikia vibaya sana juu ya kile kilichotokea. Samahani na hamtawahi kusikia chochote kibaya kutoka kwangu, kitu pekee mtakachosikia kutoka kwangu ni burudani," Omosh aliongea.

Alizidi na kuzungumza na kusema kuwa;

"Mhojiwa aliniuliza Ikiwa ningependa msaada kutoka kwa Wakenya. Ni kitu cha kupeana na kuchukua.

Pia nilikuwa nimeulizwa mapema nitasema nini ikiwa nitakutana na gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko.

Nilisema nitataka kamera, tripod, na lights. Watu wananijua kutokana na uigizaji."

Omosh pia amesema kuwa hajarejelea uraibu wa pombe na kuwa amekaa kwa muda bila kubugia vileo.