Je Diamond Platnumz ni Bill Gates ajaye?

Diamond aliombwa kusimama kama mbunge lakini akasema "hiyo sio fani yake".

Muhtasari

•Diamond Platinumz alikuwa tu amethibitisha kupokea gari lake aina ya Rolls Royce jipya kabisa, wakati BBC ikiongea naye - ni la rangi ya Cullinan buluu, toeo la hivi karibuni.

•Diamond hafadhaishwi na wakosoaji wake na anasema "hachukulii hilo kibinafsi".

Image: WASAFI

Diamond Platinumz alikuwa tu amethibitisha kupokea gari lake aina ya Rolls Royce jipya kabisa, wakati BBC ikiongea naye - ni la rangi ya Cullinan buluu, toeo la hivi karibuni.

Ni ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania na wakati Diamond alipoichukua katika safari yake ya kwanza, hebu fikiria kilichotokea.

“Kwangu mimi sio tu gari langu, ni gari letu. Yeyote aliyeniunga mkono, tusherehekee mafanikio yetu, ” Diamond alisema.

Diamond alishindwa kupata tuzo za BET huko Marekani hivi karibuni na Burna Boy akaichukua, lakini picha ya msanii huyu wa Tanzania ndio iliyokuwa imesambaa kila mahali kwasababu ya mavazi yake ya jadi ya Kimasai.

Nchini Marekani pia alikuwa akirekodi albamu mpya ambayo mtayarishaji mkuu ni Mmarekani na amewashirikisha wasanii wa Marekani.

Alichapisha picha kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na Busta Rhymes, Swizz Beats na Diddy, miongoni mwa wengine.

Hata hivyo, sio kila mtu alikuwa akimuunga mkono Diamond katika safari yake ya Marekani.

Baadhi ya watu kutoka nchi yake walisema hakustahili uteuzi wa BET kwasababu ya kumuunga mkono kwake bila sababu Rais wa zamani wa Tanzania John Pombe Magufuli.

lakini Diamond hafadhaishwi na wakosoaji wake na anasema "hachukulii hilo kibinafsi".

Diamond aliombwa kusimama kama mbunge lakini akasema "hiyo sio fani yake".

Sasa basi, Diamond anajiona akiwa wapi katika kipindi cha miaka 10 ijayo?

"Siku zote nilitaka kudhibitisha jambo kwa vijana wa Kiafrika, kwamba unaweza kutumia muziki kwa njia nzuri sana, ukatumia muziki kuajiri watu zaidi, na kuwa mmoja wa watu matajiri zaidi ulimwenguni - kama Jeff Bezos au Bill Gates", alisema.

Kwa hiyo, Diamond atakuwa anasafiri kwenda anga la mbali?

Au kutumia pesa zake kwa sababu anazoziamini?

Je! Atakuwa Jeff Bezos au Bill Gates?

“Sio mmoja wao bali atakuwa bora kuliko wao!"

“Sioni nikisafiri kwenda mwezini kwasababu ninaogopa kusafiri kwenye anga. Lakini nitawawezesha vijana. Kinachonifurahisha ni kusikia mtu akisema ni kwasababu ya Diamond ndio leo nimefika hapa, ”alisema.