- Mashabiki wamuonya Flaqo baada ya kumkejeli rappa Octopizzo
Erastus Ayieko Otieno maarufu Flaqo ni mmoja wa wasanii na wachekeshaji wengi wanaosherehekewa nchini Kenya.
Yeye ni ufafanuzi wa kweli wa kutia bidii katika kazi yake tangu alipoanza kazi ya ucheshi akawa na mafanikio zaidi kuliko watu waliokuwa katika sekta ya burudani mbele yake.
Maudhui yake kwa kawaida yanategemea masuala yanayohusiana na jamii ikiwa ni pamoja na nyumba za Afrika, shule kati ya mengine.
Flaqo alipakia video yake mwenyewe akiiga jinsi Octopizo huwa anaandika nyimbo zake.
Alitumia sauti ya Octopizzo lakini alitumia maneno ya kupendeza ili kuunda mistari.
Baadhi ya mashabiki wake walifuahishwa na video hiyo, huku wengine wakimuonya kuwa atapokea kichapo, kwa ajili ya kitendo hicho alimfanyia Octopizo.
Hizi hapa jumbe za mashabiki;
tosh_muriithi: πkijana utamadwaπ
bencyco: What's wrong with you man?πππ
bandanafather: ππutapigwaππππ
elkavio_jnr: Umeamua V for violensπππ
its_vijay_vick_the_dj: ππππsaizi ako anaandika Noma niko maganji π₯π₯π₯π₯
mr_kakerea_: Pizoo deeππ Kin'g en yu know et!π
being_ayalaa: Utagongwa msee