Mwaka wa baraka!Orodha ya watu mashuhuri waliobarikiwa na watoto mwaka wa 2021

Muhtasari
  • Lakini kuna baadhi ya watu mashuhuri ambao wanasherehekea baraka baada ya kubarikiwa na watoto
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Kubarikiwa na mtoto maishani mwa wanandoa au wapenzi ni moja wapo wa baraka tele ambazo hudumisha mapenzi katika ndoa na uhusiano.

Mwaka wa 2021 umekuwa na baraka zake na misukosuko yake kwa njia moja au nyingine.Lakini kuna baadhi ya watu mashuhuri ambao wanasherehekea baraka baada ya kubarikiwa na watoto.

Ni safari ambayo sio rahisi kwa akina mama lakini endapo amemuona mwanawe mikononi mwake hujawa na furaha tele.

Hii hapa orodha ya baadhi ya watu mshuhuri ambao walibarikiwa na watoto mwaka wa 2021;

1.Vera Sidika na Brown Mauzo

Wawili hao walibarikiwa na mtoto msichana ambaye anafahamika kama Asia, na ambaye ana urembo wa kupindukia.

Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Vera alijifungua 10/10/2021.

2.Mulamwah na Caro Sonie

Sonie alijifungua mtoto msichana Septemba 20/2021.

3.Corazon Kwamboka na Frankie

Ni wapenzi ambao wamekuwa wakionyesha mapenzi yao mitandaoni, huku wakiwa watu mashuhuri wa hivi punde kubarikiwa na mtoto msichana  mapema mwezi wa Desemba.