Eric Omondi aweka kiasi ambacho wasanii wa Kenya wanapaswa kulipwa kwa maonyesho

Muhtasari
  • Aliendelea kuorodhesha idadi ya wasanii wa orodha A ambao hawapaswi kamwe kulipwa chini ya Sh600, 000 kwa kila onyesho
eric-omondi
eric-omondi

Mcheshi Eric Omondi ametoa masharti magumu ambayo mapromota na waandaji wa hafla wanapaswa kuzingatia 2022 wanapoandaa maonyesho au tamasha.

Kulingana na Eric wasanii wote waliowekwa kwa ajili ya maonyesho lazima walipwe 75% ya kiasi kilichokubaliwa mapema na 25% iliyobaki siku ya tukio.

Aliendelea kuorodhesha idadi ya wasanii wa orodha A ambao hawapaswi kamwe kulipwa chini ya Sh600, 000 kwa kila onyesho.

“Tafadhali fahamu kuwa mwaka huu nitachunguza kibinafsi kila undani wa kila tukio!!! Nataka kujua wasanii wanalipwa kiasi gani. Ninataka kuhakikisha kuwa kila msanii analipwa asilimia 70 ya pesa zake kabla na asilimia 25 siku ya tukio kabla ya tukio

Kila msanii kwenye orodha lazima alipwe si chini ya ksh 600,000. katika orodha A inamaanisha yafuatayo.

“Nadia Mukami - KSH 600,000,Khaligraph Jones MILIONI 1.5,Otile Brown - KSH MILIONI 1.5,Nyashinski - KSH MILIONI 1.5,Sauti sol - KSH 2.8 MILIONI,” inasomeka sehemu ya chapisho la Omondi.

Aliongeza kuwa wasanii wote wa orodha ya B wanapaswa kulipwa Sh450, 000 na zaidi kwa kila shoo, akitoa mfano wa rapa mchanga na nyota wa Gengetone, Trio Mio.